Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, June 21, 2013

'SUJUTII KWA NILIEKUWA NAE' YA BARNABA VIDEONI






Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Barnaba Elias ‘Barnaba’ ameachia video ya kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Sijutii kwa niliekuwa nae’ ambacho kinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Barnaba alisema wimbo huo kaupeleka sokoni wiki iliyopita na kwamba umeshaanza kufanya vizuri katika soko hilo, kitu ambacho kinampa moyo wa kufanya kazi hiyo bila kuchoka.
“Kama kawaida yangu nyimbo zangu nyingi huwa haziwachukizi mashabiki wangu ni jambo ambalo namshukuru mungu kwani ni wasanii wachache ambao nyimbo zao zinafanya vizuri mtaani,” alisema.
Barnaba alisema anawaomba mashabiki wa muziki huo kuendelea kumpa sapoti katika kazi zake ikiwa ni pamoja na kukaa mkao wa kula kwaajili ya kupokea kazi nyingine ambazo zinakuja.
Mbali na kibao hicho, Barnaba alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Magubegube, Wrong number, Tulizana, Milele daima, Sorry na vinginevyo ambavyo vinafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini.

No comments :

Post a Comment