Na Elizabeth John
AKIWA
bado anafanya vizuri katika filamu, mwanadada Irene Paul amesema
kwamba filamu ya kibajaji ilimfanya ajifunze kuendesha chombo hicho kwa
lazima ili kuleta uhalisia.
Japo awali alisema aliona kama ingekuwa ni kazi ngumu sana
kwake lakini ilimbidi kukaza roho kwa kuwa yeye ni msanii ambaye angependa
kuwaonesha mashabiki wake vitu vya ukweli na si vya kuongopea.
Katika filamu hiyo ambayo safu hii iliichambua wiki
iliyopita, Irene ameweza kuitendea haki akiwa sambamba na mchekeshaji Salum
Haji’Mboto’ ambapo kumejaa vituko vitakavyokufanya ucheke hata kama umemka vibaya siku hiyo.
Mwanadada
huyo ni kati ya wasanii ambao wanakuja juu katika tasnia hiyo ambapo
mwaka huu amefanikiwa kuchukua tuzo ya msanii bora wa kike
anayechipukia, zilizotolewa katika ukumbi wa Ubungo Plaza wiki iliyopita
jijini Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment