Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, June 15, 2013

Watatu wafa wa bomu mkutano wa CHADEMA






Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.
Katika Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema na  Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema   hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.

Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara  tu baada ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali inayoashiria mrushaji huenda alilenga kuwajeruhi viongozi hao.

Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuawa.

Hali ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.

Kijana mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na baadae kukimbilia nyumba zilizo jirani.
DSC07403
Mbowe - SowetoMwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasili viwanja vya Soweto, Kata ya Kaloleni Jijini Arusha jioni ya leo katika Mkutano wa Chadema kufunga kampeni zake.
DSC07401Mh Mbowe akichangisha pesa mkutanoni hapo sekunde chache kabla ya mlipuko kutokea
DSC07413Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko ulioua na kujeruhi vibaya
DSC07407Hali za majeruhi na marehemu wakiwa chini kabla ya kukimbizwa hospitalini
DSC07408
:

No comments :

Post a Comment