Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali Watu cha Zantel, Francis Kiaga akifafanua jambo wakati wa ushirikiano
na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili
kuwawezesha watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa
na lengo la kupata ushauri kwa masaa 24 mahali popote nchini. Kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa BR Solutions, Richard Toba na Ofisa Biashara Mkuu wa
Zantel, Sajid Khan. (Picha na Habari Mseto Blog)
Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Dk. Aidan Njau akifafanua jambo, Sajid Khan.
DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Zantel imezindua ushirikiano na Kampuni
ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha watanzania
kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa ni kupata ushauri kwa masaa
24 mahali popote nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Zantel jijini Dar es
Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel Francis Kiaga
alisema, wameamua kuingia ubia na Wizara pamoja na BR ili kuwasaidia watumiaji
wa Zantel kuongea moja kwa moja na madaktari endapo watakuwa na tatizo linalowasumbua
ambalo wanahitaji ushauri.
“Huduma hii ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ sisi kama Zantel tunaimani
itawanufahisha watanzania kupata ushahuri kwa bei laisi juu ya matatizo
yanayowasumbua na ndio maana tumeamua kubolesha maisha ya wateja wetu kwa
teknolojia ya simu za mikononi kwa kuwa tunatambua Watanzania wengi wanatumia
simu,”alisema Kiaga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa BR Solution Francis Njau alisema,
huduma hiyo itashughulikia magonjwa kama, Ukimbi, Cancer, Moyo, Malaria, Afya
ya Uzazi na huduma ya kwanza ambayo bado wanajipanga zaidi jinsi ya
kuwafahamisha watanzania jinsi ya kufanya tofauti na kumwelekeza mgonjwa kwenda
duka la madawa bila ya kwenda hospitalini kwanza.
“Tukumbuke Zantel walishawahi kushinda tuzo za ubunifu katika kutumia
teknolojia katika kubolesha afya na huduma kupitia huduma yake ya Mobile Baby
katika tuzo la kongamano la Makampuni ya simu mwaka jana,”alisema.
Kwa upande wa Daktari Aidan Njau wa Aghakan Hospitali alisema,
wamejipanga kuhakikisha wanawapa ushauri mzuri watanzania ambao watapiga simu
au kutuma meseji ambayo itatangazwa hapo badae na kudai kuwa huduma hiyo
itakuwa sio kumpata dawa mgonjwa kwa kuwa fani yao hairuhusu kumpa mgonjwa dawa
bila ya kumpima.
“Katika kipengele cha huduma ya kwanza kuna ushahuri ambao
tutamwambia mgonjwa atakapopiga simu, ila kumwambia tumie dawa ni ngumu kwa
kuwa mtu anaweza kupiga simu anasema anaumwa kichwa ukamwambia tumie
Diklofenak alafu kumbe ana vidonda vya tumbo ambapo ni hatari
zaidi,”alisemaTumaini.
No comments :
Post a Comment