Baadhi ya Watanzania waishio Afrika Kusini wakiuaga mwili wa Ngwair (Picha kwa hisani ya deejaydeo.blogspot.com) |
Kinjekitile 'Kinje' Ngombale Mwiru (mbele) akiwa na watanzania wengine kufanya harakati za mwili wa Ngwair kurejeshwa nchini. |
BAADA ya danadana ya siku kadhaa juu ya ratiba kamili ya kuwasili kwa mwili wa msanii Albert Mangwea 'Ngwair' aliyefariki Jumanne iliyopita nchini Afrika Kusini, sasa imethibitika kuwa atatua nchini kesho mchana kabla ya mwili huo kuagwa na watanzania kwenye viwanjavya Leaders, Kinondoni.
Taarifa zilizopatikana jioni hii zinasema kuwa mwili wa msanii huyo umeagwa rasmi na watanzania waliopo nchini humo na kwamba kila kitu kimekamilika kwa ajili ya kesho kurafirishwa kuletwa Tanzania tayari kwa mazishi yatakayofanyika Alhamis katika makaburi ya eneo la Kihonda, Morogoro.
Awali kulikuwa na sintofahamu juu ya siku halisi ya mwili wa mkali huyo wa (free Style) kutokana na taarifa ya kwanza kuelezwa angetua nchini Jumamosi, kisha kuelezwa Jumapili kabla ya ratiba hiyo kuutwa asubuhi ya siku hiyo na kuelezwa ingekuwa leo au kesho.
Hata hivyo uhakika kabisa ni kwamba mwili wa nyota huyo wa albamu ya a.k.a Mimi na Ng'e utatua kesho kabla ya kuagwa jijini na kusafirishwa kwenda kuzikwa mjini Morogoro ambapo matayarisho mengine yamekamilika kwa kuhifadhi mwili wa mkali huyo aliyeenda Afrika Kusini kufanya maonyesho ya muziki na msanii mwezake M to the P, anayeendelea vyema kiafya nchini humo baadaya awali kuwa mahututi.
No comments :
Post a Comment