Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, June 11, 2013

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AFUNGUA MKUTANO WA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA TANAPA MKOANI IRINGA



1aWaziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akifungua mkutano wa Shirika la Hifadhi za Mbuga za Taifa TANAPA na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Wajibu wa vyombo vya habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za taifa unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo Ofisi za Manispaa ya Iringa, Balozi Kagasheki amewaasa wahariri wa vyombo vya habari kujadiliana kwa undani suala zima la kukomesha ujangili na jukumu la wanahabari katika mkakati huo wakishirikiana na serikali kwa ujumla kupitia taasisi za ulinzi katika mbuga za wanyama, amewataka wahariri kuwa wabunifu kwa kuandika makala na habari za kiuchunguzi ili kuibua mbinu hizo chafu na majangili ili kutokomeza ujangili huo na kupata ufumbuzi kamili wa changamoto hizo za ujangili, ameongeza kwamba wizara yake iko tayari kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wahariri na wadau mbalimbali yatakayofanikisha kupata ufumbuzi wa kutokomeza kabisa ujangili katika mbuga na pia amejiwekea utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari kila mwezi atakutana na vyombo vya habari ili kuzungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo. 2aWahariri mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakati akifungua mkutano huo. 3aWahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa makini katika kusikiliza wakati Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika mkutano huo. 4aBalozi Khamis Kagasheki akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano huo kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa 5aMkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Waziri wa Malisiali na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki.
1 Waziri wa Malisili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma wakati akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo mkoani Iringa ambako mkutano wa Wahariri wa vyombo vya habari na Shirika la Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA unafanyika. 3Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi Mazingira Ndugu James Lembeli akiingia kwenye ukumbi wa mkutano huku akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi kushoto. 4Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kulia akiwa katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli na kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma.

No comments :

Post a Comment