Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, June 3, 2013

Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge ' ajitahalisha na mpambano wake



Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge akiwa katika pozisheni
Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge akifanya mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake

kocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito wakati wa mazoezi yaliyofanyika kigogo mburahati Dar es salaam bonge anajitaalisha na mpambano wake na Bahati Mwafyelautakao fanyika wakati wa sikukuu ya Idi pili Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
kocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge jinsi ya kutupa makonde mfululizo wakati wa mazoezi yake Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

kocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito mazito Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Na Mwandishi Wetu

Bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Idi pili jijini Dar es salaam katika ukumbi wa friends Corner Manzese

akizungumzia maandalizi ya mpambano huo mtaalishaji Waziri Rosta amesema mpambano huo wa uzito wa juu umekuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwani mabondia hawo wanatafutana kwa mda mrefu sana na sasa wamekutana kwa ajili ya mchezo huo

Mpambano huo wa raundi 8 siwakukosa kwani ndio mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha uzito wa juu kwani mabondia wa uzito huu  wanaotamba viwango vyao ni vidogo ukizingatia kuwa wapo wachache nchini

aliongeza kuwa mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na wanaotamba hapa nchini

Na kwa upande wa kocha anaemnoa bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' amesema kuwa bondia wake alikuwa na manyama nyama mengi lakini kwa sasa akuna kutokana na mazoezi anayompatia kwani kwa sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka siku ya mchezo naisi mambo yatakuwa safi

No comments :

Post a Comment