Vijana waliojitokeza wakiwa kwenye foleni.
Jopo la washauri likongozwa na Marco Chali (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Dknob, Walter na mwisho kulia ni Godzila
Mmoja wa vijana akiimba mbele ya washauri.
Mmoja wa wasichana akionyesha uwezo wake.
Vijana waliojitokeza wakijiandikisha.
NaMwandishi wetu
Baada ya kuzinduliwa kwa mafanikio wiki mbili
zilizopita katika viwanja vya Mwembe Yanga, mamia ya vijana wamejitokeza
mwishoni mwa wiki hili katika viwanja ya ofisi za Zantel kuhudhuria usaili wa
Epiq Open Mic.
Huku ikiwa imebaki wiki kadhaa kabla ya kuanza kwa
msimu mya wa Epiq BSS, Zantel kwa kushirikana na Marco Chali Foundation,
wamezindua Epiq Open Mic ili kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Fursa hii, ya Epiq Open Mic, inawapa nafasi vijana
wenye vipaji vya muziki fursa ya kusikilizwa na mtayarishaji wa muziki maarufu
nchini, Marco Chali pamoja na jopo la wanamuziki kama Godzila na Dknob, ambao
wanawashauri mambo kadhaa kuhusiana na muziki wao, na huku wale wenye vipaji
zaidi wakipewa nafasi ya kurekodi na Marco Chali.
Akizungumzia Epiq Open Mic, Marco Chali anasema hii
ni fursa ya vijana kujifunza misingi ya muziki, lakini pia kuweza kurekodiwa
muziki wao.
‘Lengo
la Epiq Open Mic ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao,
kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika
muziki’ alisema Chali.
Marco
Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi ambazo
zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. Trinity kutokea
Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na wengine
wengi.
Kwa
upande wake, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel
inaaminini katika kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.
‘Muziki
ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana kampuni ya Zantel imeamua
kuwafikia vijana wote wenye vipaji na kuwapa nafasi ya kuonekana’ alisema Khan.
No comments :
Post a Comment