Watoto yatima wa kituo cha Ngeze education center kilichopo maeneo ya kinondoni kwa msisiri watajumuika na watoto wenzao katika tamasha la Raha za jana na leo linalojumuisha burudani ya bendi za muziki wa dansi.
Wasanii
nguli wa filamu na bongoflava wanaokubalika kwa watoto watakuepo
kula,kuimba na kucheza na watoto wote watakaodhulia katika tamasha hilo
amabapo kiingilio kwa watoto wadogo kitakuwa ni bure ambapo wazazi wao
watalipa kiasi cha tshs 8,000 tu.
Jumla
ya bendi sita zitapanda jukwaani moja kuonyesha ukali wake,pia zile
nyimbo mpya kutoka katika bendi hizo utazisikia zikipigwa live,bendi
hizo ni Twanga Pepeta"African Stars",Mashujaa musica Band ikiongozwa na Chalz baba " wazee wa tuzo tano",Bantu group ikiongozwa na ikiongozwa na "komandoo Hamza kalala".
Bendi zingine ni King kikii"wazee sugu",OTTU jazz band"MSONDO",King Kikii "wazee sugu" na DDC Mlimani park "SIKINDE"
tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 6 mwezi wa saba katika
viwanja vya posta vilivyopo kijitonyama jijini Dar es salaam.
Milamgo
ya viwanja hivyo itafunguliwa saa tano asubuhi ambapo michezo ya watoto
itaanza na kuisha saa kumi na mbili jioni ambapo burdani za bendi
zikiendelea mpaka usiku wa manane.
No comments :
Post a Comment