Na Elizabeth John
BAADA ya kufanya vizuri na kibao chake cha ‘Ni
wewe’, Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amin Mwinyimkuu ‘Amini’
anajipanga kuachia video ya kibao chake cha ‘Sipo nae’ kinachofanya vizuri
katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es
Salaama, Amini alisema anamshukuru mungu kazi hiyo imefanya vizuri na anaamini
itafanya vizuri kutokana na ujumbe uliopo ndani ya kibao hicho.
Alisema wimbo huo kautengeneza katika studio
ijulikanayo kwa jina la Shany chini ya mtengenezaji mahiri Mr. T ambaye
anauhakika amemtendea haki katika kazi hiyo.
“Mtayarishaji wangu namuamini sana, hivyo najua wadau wengine wataupenda
wimbo kulingana na vionjo ambavyo amevitumia mbali na ujumbe uliopo katika kazi
hiyo.” alisema Amini.
Pia aliwaomba wadau na mashabiki wa muziki
nchini kumpa sapoti katika kazi zake na wasicheze mbali na yeye kuna vitu vingi
ambavyo amewaandalia.
Licha ya kutaka kutoka na kibao hicho, Amini alishawahi
kutamba na kibao chake cha ‘Robo saa’ ambacho kilimtambulisha na kufanya vizuri
katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.
No comments :
Post a Comment