Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, November 22, 2013

HIKI NDICHO KIPAJI KIPYA ALICHOKIIBUA MWANAMUZIKI SNURA KWA KIUNGO MSHAMBULIAJI WA KLABU YA YANGA NA TAIFA STARS MRISHO HALFAN NGASSA.



Mrisho Halfan Ngassa anavyo mbebeleza mahaba ya Snura kwa kumsuka nywele.


WAKATI hali ikizidi kuwa tete nyumbani kwa mshambuliaji wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars) Mrisho Ngassa baada ya kudaiwa kuwa kumeibuka ugomvi mkubwa baina yake na mkewe.






Ugomvi huo unatokana na siri ya mahusiano ya mepenzi baina yake na Msanii wa Musiki wa Kizazi Kipya Snura Anton, maarufu kwa jina la majanga, msanii huyo amejitokeza hadharani na kudai kwamba hana mahusiano ya kimapenzi ya mwanasoka huyo. 


Tangu jana picha za wawili hao zilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, wakiwa kwenye pozi mbalimbali za mahaba huku Ngassa akigeuzwa msusi wa nywele za mwana dada huyo mwenye sifa ya kurubuni wanaume, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutumia makalio yake ipasavyo wakati wowote. 


Katika maelezo yake ambayo pia yamezagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii Snura amaesema kwamba, Ngassa ni rafiki yake tuu na si vinginevyo. 


“Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu na alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu"; 


"Tatizo ni kwamba, simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo" Ngassa ambaye anaonekana kuwa msusi mahiri wakati mahaba akionyesha kila dalili za kuchanganywa na mahaba ya kimwana huyo. 


Hata hivyo Habarimpya.com ilimtafuta Ngassa ambaye hivi sasa yuko kwenye kambi ya Taifa Stars inayojiandaa kucheza mechi ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) lakini akashindwa kusema lolote kwa madai kwamba hivi sasa hapaswi kuzungumza chochote juu ya suala hilo. 


Mwaka 2011 akiwa katika kikosi cha Azam, Ngassa aliwahi kufumaniwa akiwa na mwanamke chumbani kwake, wakati huo akiishi katika chumba kimoja maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam, tukio hilo lilimpa fedheha mshambuliaji huyo mahiri nchini Tanzania, baada ya mkewe kupiga kelele na kualika mtaa mzima nyumbani kwake kuja kushuhudia fumanizi hilo

No comments :

Post a Comment