Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, November 17, 2013

YASSIN ABDALLAH AJITOKA KATIKA TUZO BAADA YA KUKOSEKANA KWA JINA LA SUPER D KWENYE ORODHA


YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                   RAIS -TPBO                               
           taarifa rasmi-vyombo vya habari-michezo.
                       yah;- kujiondowa kuwania TUZO ya boxing award

ninayo hashima kwenu kuwafahamisha yafuatayo;

hivi karibuni kumekuwepo na taarifa ambazo zimetolewa na watu wenye nia njema kabisa ya kutaka kuuenzi mchezo wetu wa masumbwi ya kulipwa na ya ridhaa kwa kujaribu kuwapatia TUZO wanamasumbwi [mabondia] wa pande zote mbili.

lakini inaelekea wale ambao walipelekewa wazo hili hawana nia njema ya kutaka jambo hili lifanikiwe.


kwani kabla ya hata kura zenyewe kuanza kupigiwa washindani ofisi zetu za TPBO tumekuwa tukiletewa malalamiko kutoka kwa baadhi ya mabondia ambao wameachwa kuorodheshwa nan hata wadau wengine pia wameachwa na kuingizwa watu ambao hawastahili ,huu ni ubaguzi ambao sidhani kama ni lengo la waandaaji wa TUZO hizi,.niewasilisha malalamiko hayo kwa wahusika ,nao wanarushiana mpira kwamba ni kiongozi wa juu wa pst ameondowa baadhi ya majina waliyoyaweka katika orodha.


niejaribu kusoma kwa undani sana orodha ya majina ambayo nimetumiwa  ya wanaoshindanishwa katika TUZO hizo,wamo waandishi wa habari ambao TPBO inadhani wana haki ya kupewa tuzo bila kushindanishwa kwa kuwa wao ndiyo wameufanya mchezo wa masumbwi kujulikana sana miaka hii baada ya kuzimia kwa miaka takribani 7 ya nyuma kutokana na viongozi wabinafsi , ambao bado wanataka kuuingiza katika TUZO hizi.


mfano unapoyaandika majina ya watangazaji wa chombo kimoja cha habari [TV REDIO AU GAZETI na ukamuacha mmoja wao kushindania TUZO hii je huoni kama huutambuwi mchango wake ,na tayari umeshajenga matabaka kazini kwake?


nimeshtushwa sana nilipoliona jina langu la yassin abdallah ustaadh,limo kwenye kuwania tuzo ya kiongozi bora,halafu naangalia wanowania tuzo kwa upande wa waamuzi na majaji sioni jina la referii au jaji hata mmoja  kutoka TPBO ina maana hao waliowasaidia waandaaji kuwapatia majina hawawajuwi waamuzi wa tpbo au ndiyo ubaguzi?


nimeangalia pia katika 0rodha ya waandishi sijaliona jina la SUPER D COACH [Rajabu Mhamila]
  ambaye ana miliki mtandao wa habari za masumbwi wa  www.superdboxingcoach.blogspot.com  
mtandao huo umekuwa ukitujuza habari mbalimbali za masumbwi za ndani na nje ya nchi hii

bado najiuliza tena hivi hao waliowasaidia waandaaji wa TUZO hii hawamjuwi SUPER D COACH au hii TUZO imeshafanyiwa hila za kuwatenga watu muhimu katika BOXING? NANI ASIYEJUWA MCHANGO WA SUPER D KATIKA NGUMI ZA KULIPWA,NA NGUMI ZOTE KWA UJUMLA HAPA, NCHINI TANZANIA ? MPAKA ASAHAULIWE KIASI HIKI


KWA MAELEZO HAYA PEKEE INAONYESHA NI JINSI GANI WATU WANAOJIITA VIONGOZI WA NGUMI ZA KULIPWA WANAVYOTAKA KUVURUGA DHAMIRA NJEMA YA WAANDAAJI WA TUZO HIZI KWA KUWABAGUWA WATU KWA CHUKI BINAFSKI.


UAMUZI WANGU BAADA YA HAYO YOTE NINALIONDOWA JINA LANGU RASMI KUWANIA TUZO HIZI PAMOJA NA SABABU ZIFUATAZO;-


[A]TPBO-LIMITED NI KAMPUNI KUBWA [search google] NA MIMI PIA NINAYO HESHIMA KUBWA KWA WATANZANIA KWA KAZI NINAZOWAFANYIA ,HIVYO SIKO TAYARI KUSHINDANISHWA KATIKA TUZO AMBAZO HAZINA VIGEZO VYA KUSHINDANIA.


[B] TPBO-LIMITED SIYO MIMI PEKE YANGU BALI NI PAMOJA NA WAAMUZI NA VIONGOZI WENGINE PIA.


[C] TPBO-LIMITED HAIKO TAYARI KUONA WATU WANATUMIA FURSA HII YA TUZO KUPENDEKEZA MAJINA KWA LENGO LA KUWABAGUWA WENGINE KWA FANI MOJA WAZIFANYAZO NA ZINAZOFANANA.KWA SABABU ZISIZOELEWEKA.


[D] TPBO-LIMITED INAHESHIMU SANA WAZO LA WAANDAAJI WA TUZO HIZO, LAKINI HAIHESHIMU KABISA MFUMO ULIOTUMIWA NA VIONGOZI WA NGUMI WALIOPENDEKEZA MAJINA YA MABONDIA NA WADAU WENGINE ,KWANI YANAANZA KULETA MALUMBANO YASIYO YA LAZIMA.


[E]TPBO-LIMITED BILA KUBAGUWA ITAWAPATIA HATI WADAU WOTE WALIOACHWA  KWA CHUKI BINAFSI AKIWEMO SUPER D COACH KWA KUTAMBUWA MICHANGO YAO MIKUBWA WALIYOITOWA KATIKA NGUMI ZA KULIPWA.

                                AHSANTENI SANA                              IMELETWA KWENU NAMI                     YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                   RAIS -TPBO

No comments :

Post a Comment