Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, November 26, 2013

K-Guitar wa Bana Marquis wala hajutii




Kelvin Nyoni 'K Guitar' kaika pozi
MUIMBAJI wa bendi ya muziki wa dansi ya Bana Marquiz, Kelvin Nyoni 'K Guitar', amefyatua wimbo wake binafsi uitwao 'Sintojutia' uliopo katika miondoko ya Zouk.
Tayari wimbo huo umeanza kurushwa hewani na baadhi ya vituo vya redio nchini na kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kufyatua video yake ili mashabiki wapoate uhondo kamili.
Akizungumza na MICHARAZO, mwanamuziki huyo anayecharaza pia gitaa la rythm alisema wimbo huo ameurekodia katika studio za Swadt Records chini ya prodyuza T-Tach kwa msaada mkubwa wa mameneja wake watatu  akiwamo mchora katuni wa gazeti hili, Abdul King'O.
Kelvin alisema wimbo huo ni mwanzo wa safari ndefu ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki kupitia albamu yake binafsi itakayokuwa na nyimbo zaidi ya sita katikka miondoko tofauti za Zouk, Bongofleva na Rhumba.
"Baada ya kukamilisha kutoa video ndipo nitaanza kurekodi nyimbo nyingine ambapo mpaka sasa tayari ninazo kama tatu zilizokamilisha mashairi yake," alisema Kelvin.
Kelvin kabla ya kuingia kwenye muziki wa dansi akijiunga na bendi ya Bana Marquiz inayoongozwa na mwanamuziki nyota wa kimataifa, Tshimanga Assosa Kalala 'Mtoto Mzuri', alishawahi kutoa wimbo wa Bongofleva wa 'Mapenzi Siyo Pesa' kabla ya kuurudia tena katika bendi hiyo

No comments :

Post a Comment