Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, November 6, 2013

SIMBA YAINYUKA ASHANTI 4.2




Mshambuliaji wa Simba Betram Mwombeki, akidhibitiwa na beki wa Ashant United, Tumba Sued, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Simba imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 na kufikisha jumla ya Pointi 24 wakiendelea kubaki nyuma ya watani wao wa Jadi Yanga kwa tofauti ya Pointi 1.
Mshambuliaji wa Simba,Amis Tambwe,akijiandaakupiga shuti mbele ya beki wa Ashant United, Jaffari Gonga,wakati wamchezo huo. Picha na Habari Mseto
**********************************
KOCHA Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni leo ameshusha presha ya kutaka kung’olewa katika klabu hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Ashanti United katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ikitoka kutoa sare tatu dhidi ya Yanga (3-3), Coastal Union (0-0) na Kagera Sugar (1-1) na kufungwa 2-1 na Azam, Simba SC leo ilipata ushindi wake kupitia kwa Betram Mwombeki, aliyefunga mawili, Amisi Tambwe na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Pamoja na ushindi huo, Simba SC inabaki nafasi ya nne kwa pointi zake 24, baada ya kucheza mechi zote 13 za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu. 
Azam na Mbeya City zenyewe zina pointi 26 kila moja na Yanga inafuatia ikiwa na pointi zake 25, ambapo timu zote hizo zinashuka dimbani kucheza mechi zake za mwisho kesho.
Simba SC walitangulia kupata bao katika dakika ya nane kupitia kwa winga wake machachari, Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyepasua katikati ya ukuta wa Ashanti baada ya pasi ya Amisi Tambwe kabla ya kumchambua kipa mkongwe, Amani Simba. 
Ashanti walisawazisha dakika ya 45 mfungaji, Hussein Swedi aliyeunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya Hussein Mkongo kutoka wingi ya kulia.
Timu hizo zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza, Ashanti wakigonga pasi fupi fupi zenye kusisimua na Simba wakitumia mipira mirefu kushambulia kupitia kwa washambuliaji wake wawili, Tambwe na Betram Mombeki.  
Kipindi cha pili, mabadiliko yaliyofanywa na Kocha mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ kuwatoa wakongwe Henry Joseph na Amri Kiemba na kuwaingiza chipukizi Said Ndemla na William Lucian ‘Gallas’ yaliisaidia Simba kupata ushindi.
Amisi Tambwe alifunga bao la pili dakika ya 46 tu akipokea pasi ya Singano ‘Messi’ na Mombeki akafunga la tatu dakika ya 50, akiunganisha krosi ya Haruna Shamte. 
Mkongwe Said Maulid ‘SMG’ aliifungia Ashanti bao la pili dakika ya 53 kwa pasi ya Hussein Swedi, lakini Mombeki akaihakikishia Simba SC ushindi kwa bao zuri dakika ya 61 akiunganisha krosi ya Shamte tena.
Simba SC ingepeta mabao zaidi kama ingeweza kutumia nafasi zaidi ya mbili nzuri ilizotengeneza. Kipa Amani Simba alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 90 baada ya kudakia nje ya eneo lake mpira. Nahodha Paul Maona alimpisha kipa Daudi Mwasongwe akamalizie mchezo. 
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abuu Hashimu, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Gilbert Kaze, Hassan Hatibu/Hassan Isihaka dk75, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’, Henry Joseph/Said Ndemla dk46, Betram Mombeki, Amisi Tambwe na Amri Kiemba/William Lucian dk46. 

Ashanti United; Amani Simba, Hussein Mkongo, Jaffar Gonga, Tumba Swedi, Samir Ruhava, Iddi Said, Fakih Hakika, Paul Maona/Daudi Mwasongwe dk90, Hussein Swedi, Said Maulid ‘SMG’/Abdul  Kimbirwa dk83 na Joseph Mahundi.

No comments :

Post a Comment