Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, February 7, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI MPYA WA OMAN NCHINI TANZANIA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Oman nchini Tanzania, Soud Ali Mohamed Al Ruqaishi, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 7, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi mpya wa Oman nchini Tanzania, Soud Ali Mohamed Al Ruqaishi, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 7. Picha na OMR.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amempokea Balozi mpya wa Oman nchini Tanzania Balozi Soud Ali Mohamed Al Ruqaishi ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam na kisha kufanya naye mazungumzo. Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais amemhakikishia Balozi Ruqaishi kuwa Tanzania na Oman zina uhusiano wa kindugu wa siku nyingi na kwamba uhusiano huo umekuwa ukinufaisha nchi hizi kwa miaka kadhaa.

Mheshimiwa Makamu wa Rais aliendelea kufafanua kuwa, Tanzania kwa sasa inashirikiana na Oman kiuchumi na kwamba kuna wawekezaji wengi kutoka Oman ambao wako nchini, sambamba na wengine wanaoonesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali hapa Tanzania.

Kwa upande wake Balozi Ruqaishi alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, Oman inafurahia uhusiano wake na Tanzania na kwamba jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha kuwa uhusiano huo unadumu na kunufaisha nchi hizi mbili. Pili alifafanua kuwa, atahakikisha katika kipindi chake cha Ubalozi hapa Tanzania anasaidia kutanua fursa za uwekezaji kwa wawekezaji kutoka Oman sambamba na kuwafungulia fursa kama hizo wawekezaji walio na nia ya kuwekeza nchini Tanzania.

Oman licha ya kuwa na uhusiano wa karibu na Tanzania na hasa Visiwani Zanzibar, inabakia kuwa ndiyo nchi pekee duniani nje ya Afrika iliyo na wazungumzaji wengi wa lugha ya Kiswahili. Katika siku za hivi karibuni, wawekezaji kutoka Oman wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya Mafuta na Gesi sambamba na kuliimarisha shirika la Ndege Tanzania ili limudu ushindani na kuongeza ufanisi wa shughuli zake katika biashara ya safari za anga.

Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam, Ijumaa Februari 07, 2014

No comments :

Post a Comment