Pichani ni mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe
akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kawe,Halima Mdee wakiwa
wameachiwa na jeshi la polisi akisindikizwa kwenda kupanda chopa katika
viwanja vya mwembetogwa mara baada ya kudaiwa kuzidisha muda kwenye
mkutano wao wa hadhara mkoani Iringa. (picha zote na denis mlowe)
MBOWE ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI IRINGA.
Na Denis Mlowe,Iringa
MWENYEKITI
wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa jimbo la Hai na Mbunge wa Jimbo
la Kawe Halima Mdee walishikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu
Iringa, kwa kosa linalosemekana kuzidisha muda wa mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mgama wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.
Kwa
majibu wa Mbowe alisema jeshi la polisi walimshikilia kwa masaa mawili
kwa mahojiano na mkuu wa kituo cha polisi na kisha kumwachia huru.
Akizungumza
na wafuasi wa Chadema kabla ya kupanda Helkopta na kuelekea mkoa wa
Pwani akiambatana na Mbunge wa Kawe Halima Mdee aliwataka wananchama wa
Chadema kuungana katika kukijenga chama bila hofu na kuwashukuru kwa
kuwaunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi.
Alisema
wakati wanajiandaa kuondoka alipata malalamiko kutoka kwa kamanda wa
Polisi wa Wilaya kuwa wamezidisha muda wa kufanya mkutano katika kijiji
hicho.
Mbowe
alisema kuwa chanzo kingine ni baadhi ya viongozi wa kijiji
kuwadanganya wananchi katika mkutano uliotakiwa kufanyika katika vijiji
vya kata ya Ukumbi kuwa watakuwepo wabunge na mwenyekiti wa chama
katika mkutano kitu kilichosababisha kuwepo na dalili za ugomvi.
“Jeshi
la polisi limetuhoji kuhusu mambo hayo na baada ya kuwaeleza
walituachia huru na ila wamesema wakituhitaji watatuita lakini makamanda
naomba sana mjenge chama na nawashukuru sana kwa kutuunga mkono katika
harakati za kuikomboa nchi” Alisema Mbowe.
No comments :
Post a Comment