Mbunge wa iringa mjini-chadema Mchungaji Peter Msigwa
--
Napenda kuchukua nafasi hii kama waziri kivuli wa
maliasili na utalii katika kuishinikiza Serikali hasa waziri wa
maliasili na utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu kutoa majibu ya maswali magumu
ambayo si Tanzania tu pekee inayahitaji lakini pia Jumuia ya kimataifa
inayahitaji kuhusu kukithiri kwa tatizo la Ujangili nchini hasa kwa
wanyama jamii ya Tembo na Faru.
Hivi karibuni gazeti la Daily Mail linalochapishwa nchini Uingereza liliripoti kuhusu biashara haramu ya pembe za ndovu ambayo inakadiriiwa kuwa na soko la shilingi trilioni 19 za kitanzania.
Pamoja na majibu ya waziri Nyalandu ambayo yalilenga kuhaminisha watanzania kuwa taarifa ile imelenga kuchafua Tanzania, anasahau kuwa huo ndio ukweli halisi kuwa Tanzania sasa imejichafua yenyewe kwenye taswira ya kimataifa kwa citendo hivyo haramu.
Labda waziri Nyalandu anasahau kuwa, ulimwengu wa sasa ni wa kiteknolojia ambapo taarifa mbalimbali juu ya biashara haramu ya pembe za ndovu pamoja na mauaji ya tembo, yamesambaa kila mahali hasa katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi ikiwemo mitandao mbalimbali ya kimawasiliano.
Leo hii wakati waziri akitumia nguvu nyingi kupangua tuhuma dhidi ya Serikali katika kushindwa kwake kuangamiza biashara hii haramu, anassahau pia takwimu za serikali zinaonesha kuwa mwaka 2010 tembo 10000 waliuwawa Tanzania pekee. Hii ni wastani wa tembo 37 kwa siku. Hivi sasa Tanzania ina tembo kati ya 150,000 na 170,000 . ina maana kuwa mpaka kufikia mwaka 2017/2018 Tanzania inaweza isiwe na tembo hata mmoja. Kwa takwimu hizi, waziri anawezaje kusema kuwa Serikali inachafuliwa?
Mara kadhaa pia, waziri Nyalandu amekua akikaririwa kuwa mtandao wa Ujangili ni mpana na wenye nguvu za pesa, kisiasa na kimamlaka. Na pia amekaririwa akiwasihi wanaojihusisha na shughuli za Ujangili waache mara moja kwani serikali inawajua. Swali, unawezaje kumbembeleza mtuhumiwa huku ukijua anavunja sheria za nchi? Je kuna watu ambao katika nchi inayojisifu kuwa na utawala bora, wako juu ya sheria na hawaguswi na sheria?
Majibu haya ya waziri, yanadhihirisha kuwa mtandao huu unaolalamikiwa na kuogopwa ndo unahousisha Ikulu, wanasiasa, watumishi wa Serikali, maafisa wanyamapori,maafisa usalama, polisi, wanajeshi na wafanyabiahsara wakubwa ambao wamekua wakihushishwa na Serikali hii ya CCM.
Kambi rasmi ya upinzani katika hotuba zake za bajeti na michango ya mara kwa mara, imekua ikitoa msimamo wake ikiwa ni pamoja na kuwataja baadhi ya watuhumiwa wa Ujangili na vidhibiti vinavyoonesha biashara haramu dhidi ya tembo inavyofanywa. Je , waziri anaweza kutueleza kuwa ameshirikiana vipi na Kambi ya Upinzani katika kushughulikia watuhumiwa hao, ikiwemo kufanya upelelezi na kujidhihirisha kama watuhumiwa hao wana au hawana hatia?
Waziri Nyalandu, akiwa na dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sera na sheria za nchi katika wizara yake ya Maliasili na utalii, wamechukua jitihada gani zaidi ya kukamata meno na pembe za ndovu au faru? Vipi kuhusu kuzuia zaidi wanyama hao wasipotee katika sura ya taifa letu? Je waziri anayo habari kuwa kituo cha ITV cha Uingereza, kiliweza kurekodi jinsi mtandao wa Ujangili unavyofanya kazi katika Tanzania mpaka China? Serikali imechukua hatua gani kufuatilia habari hiyo ya kipelelezi na kuwatia hatiani watuhumiwa walioonekana wakifanikisha upatikanaji wa pembe za ndovu pamoja na ahadi za kupata pembe nyengine kwa dau kubwa?
Pamoja na Serikali kuona jambo hili ni dogo, lakini wanasahau kuwa jumuia ya kimataifa hipo makini katika kulinda viumbe hai vilivyo hatarini kupotea. Kutokana na kitendo cha waziri mwenye dhamana kushindwa kujibu tuhuma nzito kama zinazotolewa na vyombo vya habari za kimataifa na kuishia kutoa maneno yasiyokuwa na ushahidi ama vielelezo vyovyote vile kwa umma ni dalili za wazi kuwa tuhuma hizo zina ukweli na ni muendelezo wa ukweli ambao niliutoa Bungeni mwaka 2012 kwa kutaja jina na Meli ambayo ilihusika kubebea shehena ya Meno ya Tembo ambayo wakala wa Meli hiyo ni Katibu Mkuu wa CCM Kinana.
Katika tuhuma hizo nzito serikali ya Tanzania imetuhumiwa kwenye mambo mazito yafuatayo na ambayo hayajatolewa majibu na Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kuwa hana majibu kutokana na ukweli wa taarifa zenyewe
Tuhuma hizo nzito na ambazo ni lazima zipatiwe majibu ya kina na tunataka kupata majibu ni kama ifuatavyo ;
1. Kuwa watu walio karibu na Mhe. Rais Kikwete wanahusika katika biashara hii haramu ya meno ya Tembo ndio maana serikali yake haichukui hatua stahiki katika kukabiliana na jambo hilo
2. Kuwa Ndege iliyomleta rais wa China Mwaka jana iliondoka na shehena ya Meno ya Tembo ambayo ilipakiwa na Maafisa waliokuwamo kwenye ndege hiyo
3. CCM na serikali yake ni wanufaika wakubwa wa mradi huu kwani wanatafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao ndio maana hawachukui hatua kwa wahusika ambao wanajulikana kwa majina na wapo mitaani wakiendelea na biashara hiyo haramu
4. Wanasiasa wa ngazi za juu katika serikali ni wahusika wa moja kwa moja katika biashara hii haramu na wapo Wabunge kutoka CCM ambao ni wahusika wa biashara hii.
5. Je ni kweli kuwa vitendo vya Ujangili vimeongezeka kwa kasi katika utawala wa Kikwete kuliko waliomtangulia?

Tunamtaka waziri Nyalandu atoe majibu ya kina na yakuridhisha kuhusiana na tuhuma hizo nzito kwa vielelezo na sio kwa kuishia kusema hizo ni taarifa za uongo bila kuonyesha zipi ni taarifa za kweli , na akumbuke kuwa tuhuma hizi hazijaanza kutolewa leo au jana kwani hata mini nilizitoa kwenye Bunge wakati nawasilisha hotuba ya waziri kivuli wa maliasili na utalii, pia kuna ushahidi na vielelezo viilivyotolewa na kamati ya Bunge iliyoongozwa na James Lembeli (na hapo taarifa ilisema kuna wabunge wanahusika na vigogo wa Serikali) mbona hakuwahi kusema kuwa taarifa zote hizo zilikuwa ni za uongo? Na mpaka sasa wamechunguza tuhuma ngapi?
Imetolewa na
………………….
Mhe. Mch. Peter S. Msigwa(MB),
Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii
No comments :
Post a Comment