Naibu
Waziri Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Mhe. Charles Kitwanga
(wa tatu kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Menjeja wa Bandari
ya Mtwara (wa pili kutoka kushoto) Bw. Absalim Bohella. Anayefuatia ni
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Wilman Kapenjama Ndile, na uongozi wa Mkoa
mara baada ya kupokea Shehena ya mwisho ya Mabomba ya Gesi katika
bandari ya Mtwara.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara wakiendelea na kazi ya kupakua
shehena ya mabomba ya gesi kutoka katika meli baada ya mabomba hayo
kuwasili katika Bandari ya Mtwara.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara wakiendelea na kazi ya kupakua
shehena ya mabomba ya gesi kutoka katika meli baada ya mabomba hayo
kuwasili katika Bandari ya Mtwara.
Mtaalamu
wa Masuala ya Gesi na Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya Kusafisha Gesi
Mhandisi Sultan Pwaga (katikati) akimweleza jambo Naibu Waziri wa
Nishati na Madini Mhe. Charles Kitwanga na ujumbe wake alipotembelea
eneo hilo kuangalia namna shughuli mbalimbali zinavyoendelea katika eneo
hilo.
Naibu
Waziri Mhe. Charles Kitwanga (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Wilaya
ya Mtwara Mhe. Wilman Kapenjama Ndile, (wa kwanza kulia) wakipata
maelezo kutoka kwa mtaalamu Abshakim Marunda kuhusu namna kisima cha
gesi cha nchi Kavu kinavyofanya kazi. Kwa mujibu wa Maelezo ya Mjiologia
Mwandamizi wa TPDC Bw.George Ngwale hayupo pichani ameeleza kuwa, Mnazi
Bay ina jumla ya visima vitano kati ya hivyo visima vine vina gesi
inayochimbwa na kisima kimoja kikavu. Aidha gesi inayopatikana katika
eneo hili inauzwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambao wanatumia
kuzalisha umeme unaosambazwa katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Wa kwanza
kushoto ni Katibu wa Mhe. Naibu Waziri Bw. Mjengwa Ngereja.
========= =========
========== ======== ========
NAIBU
WAZIRI CHARLES KITWANGA APOKEA SHEHENA YA MWISHO YA MABOMBA YA GESI
Na Asteria
Muhozya, Mtwara
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Mhe. Charles Kitwanga,
amepokea Shehena ya mwisho ya mabomba ya gesi katika bandari ya Mtwara na
kueleza kuwa, ujio wa miundo mbinu hiyo ni neema kwa uchumi wa Tanzania.
Aliongeza
kuwa, hiyo ni hatua kubwa katika kufikia malengo tarajiwa ikizingatiwa kwamba,
kukamilika kwa mradi huo kutachochea na kufungua njia mbalimbali za uchumi unaoendana
na sekta ya gesi na mafuta.
“Ujenzi
wa miundombinu ya kusafirisha gesi ni jambo jema kwa Tanzania, tunataka kuingia
katika uchumi wa kati wa dola elfu tatu au karibu ya hapo, tunataka pato la
mtanzania liongezeke. Sasa bila kuwa na umeme haya yote hatutayafikia. Gesi
itazalisha mengi, tunataka tufikie lengo letu. Alisema.’’ Mhe. Kitwanga.
Aidha,
aliongeza kuwa, kuzalishwa kwa gesi na kusambazwa
katika maeneo mbalimbali chini kutasaidia kufungua fursa nyingi ikiwemo kuongezeka kwa viwanda ambavyo vitakuwa na
uhakika wa kupata umeme unaotokana na
gesi.
Vilevile,
alieleza kuwa, mbali na matumizi ya viwandani gesi inatarajiwa kutumiwa katika
mahitataji mbalimbali yakiwemo matumizi ya majumbani.
“Nataka kuwaeleza wana Mtwara, si kwamba gesi
itachukuliwa yote, hapana. Tunachotaka kufanya ni kuisambaza maeneo mbalimbali
lengo letu ni kukuza uchumi wetu kwa kutumia gesi hata Mtwara viwanda vitajengwa
na fursa mbalimbali zitakuwepo”. Alisema.
Akieleza mafanikio ambayo yamekuwepo kutokana na shughuli za gesi kutumia
bandari ya Mtwara, Meneja wa Bandari Bw. Absalim Bohella alieleza kuwa, ujio wa
gesi na mradi unaotekelezwa Mkoani humo umekuwa neema kwa bandari hiyo kutokana
na kuongezeka kwa mapato yanayotokana na bandari hiyo pia kutumiwa kwa shughuli mbalimbali za gesi.
Aliongeza kuwa, tayari bandari ya Mtwara imevuka malengo ya ukusanyaji
mapato waliojiwekea ambapo hadi sasa tayari zaidi ya Tsh. Milioni mia tano
kimekusanywa.
Aidha, aliongeza kuwa, mradi wa gesi umewaongezea watumishi wa bandari
hiyo ujuzi kutokana kufanya shughuli tofauti tofauti zinazohusiana na gesi
ikiwemo upakuaji wa bidhaa zinazopitia katika bandari hiyo kwa shughuli.
“Bandari bila rasilimali watu si kitu. Kwa wafanyakazi waliobobea
wamepata ujuzi zaidi na sasa wanao uwezo wa kuhudumia shughuli zote za
bandari”. Aliongeza.
Akielezea hatua mbalimbali ambazo zimefikiwa katika ujenzi wa
miundombinu ya gesi, Mtaalamu wa Masuala ya Gesi na Msimamizi Mkuu wa Mitambo
ya Kusafisha Gesi Mhandisi Sultan Pwaga alieleza kuwa, shughuli za uwekaji mabomba
ya gesi unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Julai, 2014 ambapo pia inatarajiwa
mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu shughuli za usimikaji mitambo utakamilika.
Vile vile, ameongeza kuwa,
shehena hiyo iliyopokelewa katika bandari ya Mtwara ni ya mwisho lakini mabomba
ya mwisho ya mradi yatapokelewa tarehe 10 Februari, 2014 katika bandari ya Dar
es Salaam.
Aidha, aliongeza kuwa, miundombinu hiyo ndio kichocheo cha gesi asilia
na lengo la mradi huo ni kuhakikisha kuwa, mitambo inajengwa mahali ambapo gesi
asilia inachimbwa.
Mbali ya kupokea Shehena za mabomba ya mwisho ya gesi, Mhe. Kitwanga
ametembelea eneo la Mnazi Bay ambako gesi asilia na kuuzwa katika Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) ambapo shirika hilo linaitumia gesi hiyo kuzalisha
umeme kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Vilevile, Mhe. Kitwanga alitembelea katika eneo la Madimba kunakojengwa
kambi za wafanyakazi na panapotarajiwa kujengwa mitambo ya kusafisha gesi.
No comments :
Post a Comment