Askari Polisi wakiwa eneo la tukio ikiwa ni kuimarisha ulinzi (Picha Zote na demasho.com)
Eneo la tukio likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akizungumza jambo na waandishi wa habari
katika hoptal ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao
Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma.
Aliye lala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo.
Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa kazini.
ASKARI
watatu wa jeshi la Polisi wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Ruvuma (Homso) iliyopo mjini songea Mkoani humo wakiwa wanapatiwa
matibabu ya majeraha ambayo waliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu
kinachodhaniwa kuwa ni Bomu la kurushwa kwa mkono.
Tukio
hilo limetokea September 16, 2014 majira ya saa moja na nusu jioni
katika kata ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea
Mkoani Ruvuma ambapo watu watatu wasiofahamika walitupa kitu
kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa
kienyeji na kuwajeruhi askari hao watatu waliokuwa doria.
Askari
hao waliojeruhiwa ni WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia
kwenye unyayo na pajani ,G. 7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa
kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na G. 5515 pc John
aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo
tumboni.
Mganga
mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela ameeleza kutoa
vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa
wanaendelea na matibabu.
Alisema
kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea na
uchunguzi wa kina ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi
za kisheria. Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi Mwambungu kasema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusudi na amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.
No comments :
Post a Comment