HATIMAE CHADEMA Mkoa wa Morogoro kimepata safu mpya ya uongozi huku Susan Kiwanga akifanikiwa kutetea nafasi ya uenyekiti.
Akisoma matokeo ya uchaguzi huo mbele ya wandishi wa habari, Msimamizi wa uchaguzi huo na Katibu wa Kanda ya Kati kichama, Emmanuel Yohana, alimtangaza Susan mshindi kwa kura 26 dhidi ya 23 za Bathoromeo Tarimo.
Nafasi ya Mwenyekiti ilikuwa na wagombea wanne, Dastani Mwendi, James Mabula, Batholomeo Tarimo na Susan Kiwanga.
“Mzunguko wa kwanza Susan alipata kura 21 na Tarimo 20, hivyo kwa kuwa hazikufikia nusu ya kura zote tukarudia kupiga, ndipo tukampata Susan,” alifafanua Yohana.
Kwa upande wa nafasi ya Uenyekiti Baraza la Wazee, Aqulin Magalambula alishinda, Bavicha Barnaba Patricia na Bawacha ni Imelda Maleli.
Akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua, Susan alisema, kuanzia sasa hakuna kulala kwa kuanza operesheni maalumu ya mtu kwa mtu, nyumba kwa nyumba kushawishi kwa vielelezo, ubora wa chama na kujipanga kupata viti vya viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa.
Alisema mpango wa chama ni kuhakikisha kinakua kwa kasi ya ajabu na kutimiza dira ya chama kuelekea Ikulu 2015.TANZANIA DAIMA
No comments :
Post a Comment