Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa PST, Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, Anthony Rutta, Yazidu atazipiga na Djamel Dahou wa Algeria katika pambano la kuwania ubingwa wa Dunia wa WBO la raundi 12 na Alibaba atapigana na Alick Mwenda wa Malawi kuwania ubingwa wa UBO Afrika litakalokuwa la raundi 10.
Michezo yote pamoja na ile ya utangulizi ipatayo 10 itachezwa siku ya Septemba 12 kwenye ukumbi wa YMCA, Moshi mkoani Kilimanjaro chini ya kampuni ya Green Hill Promotion na kusimamiwa na PST.
Rutta alisema maandalizi ya michezo hiyo imekamilika na kuwataka wakazi wa Moshi na mikoa ya jirani kujiandaa kupata burudani ikiwa ni kwa mara ya kwanza kushuhudia ngumi za kulipwa katika hadhi ya kimataifa kama hiyo.
Katibu huyo alisema mbali na michezo hiyo ya kimataifa ya kuwania mataji ya UBO, siku hiyo kutakuwa 'vita' vingine kwa mabondia wa mikoa tofauti ikiwamo wenyeji Kilimanjaro katika michezo ya utangulizii ya kuwasindikiza akina Yazidu na Alibaba.
Rutta aliyataja mapambano hayo ni lile la wanadada Fatuma Yazidu wa Dar atakayepigana na Joyce Adam wa Dodoma, Emmanuel Alex wa Kilimanjaro dhidi ya Ali
No comments :
Post a Comment