Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, September 7, 2014

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA CHAKULA CHA JIONI CHA KAMPENI ZA KUPAMBANA NA UTUMIKISHWAJI WA WATOTO



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiingia kwenye kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena kwa ajili ya chakula cha jioni cha kampeni za kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa nchini kilichoandaliwa na Shirika la International Rescue Committee tarehe 5.9.2014.

Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Msanii maarufu wa kimataifa Daniele de Niese anayetumiwa na Shirika la International Rescue Committee katika kuhamasisha mapambano ya utumikishwaji wa watoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Dkt Augustine Mahiga wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na International Rescue Committee kwenye hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014 kwa ajili ya kuhamasisha mapambano dhidi ya utumikishwaji wa watoto hapa nchini.
Msanii wa Kimataifa anayetumia kipaji chake cha kuimba Daniele de Niese akiimba nyimbo mbalimbali kwa lugha mbalimbali, kiingereza, kifaransa, kitaliano wakati wa chakula cha jioni katika kuhamasisha mapambano dhidi ya utumikishwaji wa watoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza msanii wa kimataifa Daniele de Niese mara baada ya kutumbuiza kwa nyimbo zake za kusisimua kuhusu mapambano dhidi ya utumikishwaji wa watoto wakati wa chakula cha jioni kwenye Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.
Mtoto Hamadi Hatibu, 13, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi ya Sahare katika Manispaa ya Tanga akitoa ushuhuda wake jinsi alivyoishi kwa kuvua samaki katika umri wake mdogo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa chakula cha jioni cha kampeni za kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania kilichoandaliwa na International Rescue Committee kwenye Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.

No comments :

Post a Comment