Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, May 15, 2014

AMINA NGALUMA AFARIKI DUNIA NCHINI THAILAND AKIFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA



Aliyewahi kuwa mwanamuziki wa dansi wa bendi za African Revolution 'Wana tam tam' na Double M, enzi hizo chini ya uongozi wa Muumin Mwinjuma, Amina Ngalum A.K.A Japanese (pichani enzi za uhai wake) amefariki dunia nchini Thailand, ambako alikuwa akifanya shughuli zake za kimuziki.

Akizungumza na mtandao huu, mtoaji wa habari hizi, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wake katika bendi ya Tam Tam, Asha Baraka, amesema kuwa Amina amefariki dunia wakati akifanyiwa upasuaji.

''Imeelezwa kuwa Amina alianza kuugua ghafla, huku akilalamika kuwa kichwa kinamuuna na tumbo, na ndipo alipokwenda hospitali kwa ajili ya kupima na kuambiwa kua alikuwa na uvimbe kichwani na hivyo kutakiwa kufanyiwa upasuaji,

Aidha ilielezwa kuwa uvimbe huo ulikuwa ukitoa damu na baada ya kuanza kufanyiwa upasuaji hakuweza kuamka tena na ndipo umauti ulipomfika''. alisema Asha Baraka.

Mpaka mauti yanamfika, Amina alikuwa mwanamuziki wa bendi ya Jambo Survivors. Msiba upo Kipunguni B, Machimbo jijini Dar es Salaam. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMINA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

No comments :

Post a Comment