Mkurugenzi
Mkuu wa Elite learning institute Co, Hassan Kashoba (Kushoto)
akizungumzia udhamini wake kwa Taswa FC na Taswa queens. Kulia ni
mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.
****************************************************
Na Mwandishi wetu, Dar
Dar
es Salaam. Chuo bora cha Elite Learning cha Mtoni Kijichi kimeahidi
kusaidia timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo
nchini (Taswa SC) ili ziweze kusonga mbele katika shughuli zake.
Ahadi
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Elite learning institute Co,
Hassan Kashoba baada ya kuvutiwa na jinsi waandishi wa habari
wanavyojishughulisha kwa vitendo katika shughuli zao za kila siku.
Kashoba
alisema kuwa wao mbali ya kusaidia vifaa vya michezo, pia wametoa ofa
kwa waandishi wa habari wa Taswa SC kupata mafunzo ya Information and
Communication Technology (Tehama), hotel, ualimu wa shule za awali na
kompyuta.
Alisema
kuwa wanajua kuwa waandishi wana taaluma ambayo wanaifanyia kazi,
lakini katika maisha ya sasa, lazima uwe na elimu ya ziada ambayo
itakuwezesha kufanya kazi nyingine mbali ya uandishi wa habari.
“Hii ni fursa kwa waandishi wa habari wa
Taswa SC, tumeona jinsi gani walivyo mstari wa mbele katika michezo,
tena kwa kufanya kwa vitendo, sisi kwa vile tumebobea katika elimu,
tumewapa ofa hiyo, ni jukumu lao kuikubali au kuikataa,” alisema
Kashoba.
Aliongeza
kuwa kwa muda wa miaka mitatu sasa, wameweza kutoa elimu bora kwa
wanafunzi wengi wao wamepata ajira na kuamua kupanua wigo kwa waandishi.
Mwenyekiti
wa Taswa SC, Majuto Omary alikishukuru chuo hicho kwa malengo hayo na
kuwaomba watimize ili wachezaji wake waweze kutumia vifaa hivyo kwa
michezo na kusomea fani nyingine pia.
No comments :
Post a Comment