Seleman |
Dar es Salaam,
Bondia mzoefu wa ngumi za kulipwa nchini, Suleiman Galile ”tall”
anategemea kupanda tena ulingoni Mei 24 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese
jijini Dar es Salaam, kuzipiga na Abdalah Pazi “dula mbabe/kiroba” katika
pambano lisilo la ubingwa la uzito wa kg76.
Akithibitisha kuwepo kwa pambano hilo, Katibu wa ngumi za kulipwa
nchini, ambaye ndiye anayesimamia mapambano yote ya utangulizi, Bw.
Ibrahim Abbas Kamwe alisema, Galile na Dula wamekubaliana kusheza siku
hiyo ya Jumamosi ya Mei 24, huku wakisindikizwa na Karama Nyilawila na Said Mbelwa.
Watakaogombania ubingwa wa UBO,hapo awali ilipangwa Karama
kuzipiga na Thomas Mashali ambae amepatwa na majeraha kutokana na ajali ya gari.
Pia siku hiyo kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi
yenye ushindani , wakati Adam Ngange akimkabili Alan kamote wa Tanga,
zumba kukwe atazipiga na kamanda wa makamanda,Seleman Zugo na Manyenza, Ramadhan
Kumbele ataoneshana umwamba na Hassan Kiwale “Moro best”, wakati Bakari Dunda atapambana
na Mbena Rajabu.
Madogo wanaokuja juu kwa kasi katika ngumi, Idd Athuman atacheza
na Julias Thomas Kisarawe, wakati Mwaite Juma atachuana na Daudi Giligili.
Kamwe alimaliza kwa kusema
mpaka sasa hakuna bondia mwenye matatizo wote wapo katika hali ya ushindani
wanaisubiria kwa hamu hiyo siku ifikie wabanjuane kiukweliukweli .
No comments :
Post a Comment