Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, May 24, 2014

MKWE HUNA NIDHAMU', SASA NI KUFURU AUNT EZEKIEL KUWATUSI WAKWEZE


http://api.ning.com/files/UytU4r62uFOtZVuX3rs5B2YGejkdzDHgaqtgHOKytTyEyRA1G3YmanQA9KfaY0yNmFfF4bdWy2mDEf0KA0HOsMbT45Bd2zD-/auntezekiel.JPG?width=650Na : Musa mateja, Dar
NYOTA wa Bongo Movie na muigizaji mahiri nchini katika Filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson 'Jujuman' amewaacha watu hoi baada ya kuonesha dharau kwa upande wake wa pili baada ya kuwabwatukia wakwe zake aliposikia kuwa wana mpango wa kumpa talaka ili aachane na mumewe Sunday Demonte kutokana na tabia yake kwa kuwa siyo mwanamke wa kuoa (wife material). 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizo jijini Dar, Aunt alidai kuwa alikerwa na jambo hilo na kujikuta akishindwa kujizuia na kuwawakia kuwa hajaolewa na ndugu hivyo mwenye mamlaka ya kutoa talaka ni mumewe pekee.
Aunt alisema kwamba, amekuwa akisikia mara kwa mara habari za ndugu wa Demonte wakiongea maneno mengi ya kumfitinisha na mumewe.

Aidha alidai kuwa pamoja na mapungufu lakini pia ana haki zake kama binadamu hivyo jambo hilo limekuwa likimkera kwa sababu  wanaongea maneno hayo pembeni na kwamba hakuna hata mmoja aliyewahi kumfuata na kumwambia juu ya suala hilo. 

Aunt aliongeza kuwa zaidi amekuwa akiambiwa na watu wengine tu.
Akifafanua zaidi, Aunt alisema kwamba anawashangaa hao wanaojiita ndugu wa Demonte kuendelea kumtolea maneno ya kejeli kila kukicha na wakati kama wanahisi kuna tatizo kati yake na mumewe wangeweza kumtafuta na kuzungumza naye.

Alitiririka kuwa jambo ambalo halimpendezi ni pale anapokutana na watu wakimtuhumu kwamba eti ndugu wa mumewe wanataka kumpatia talaka.
“Ujue hao ndugu wanaotaka kunipa talaka wanatakiwa waelewe kuwa mimi sijaolewa na wao, hivyo hata jukumu la kunipa talaka siyo lao, maana niko vizuri na mume wangu, wala hatujawahi kukwaruzana hata kuambiana ishu za kupeana talaka,” alisema Aunt.
Ndoa ya Aunt imekuwa ikisengenywa tangu ilipofungwa mwezi June, 2012 kufutia staa huyo kutoishi pamoja na mumewe ambaye inasemekana anaishi Dubai.

No comments :

Post a Comment