RAIS
wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ yuko ndani ya bifu zito na
mwanamuziki kiwango cha juu kutoka nchini Kenya, Jackson Ngechu Makini
‘Prezzo’ chanzo kikidaiwa ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.
Bifu
la wawili hao limekuja kufuatia madai kwamba, Prezzo amemtundika Diamond
kwenye mtandao akimkejeli kwa kitendo chake cha kurudiana na Wema na
kuweka mambo hadharani.
Ilidaiwa
kuwa katika maneno yake, Prezzo alikandia akisema anamshangaa Diamond
anatamba kuwa ana mpenzi supastaa ambaye ni Wema wakati yeye mwenyewe
alishaanguka naye.
Madai
yanazidi kusema kuwa Prezzo akaongeza kwa kuandika kwamba, Bongo hakuna
mademu masupastaa kwani hata Jokate (Mwegelo) aliyewahi kutamba naye si
lolote kwake.
Msanii
huyo anadaiwa alikwenda mbele zaidi kwa kusema kama ni ustaa anao yeye
mwenye pesa zake na si Diamond ambaye hamfikii kwa lolote.
MASHABIKI WA DIAMOND WAJA JUU
Baada
ya kuanika maneno hayo yaliyoonekana kujaa kejeli, mashabiki wa Diamond
walimshukia Prezzo na kuanza kumnanga kwa kila mtu anavyoweza mwenyewe
ndipo akaanza kuhaha kutaka suluhu kwa Diamond akimuomba meneja wake
awakutanishe.
DIAMOND NAYE AWA MBOGO
Akizungumza
kwa hasira na paparazi wetu usiku wa kuamkia Mei 11, mwaka huu ndani ya
Ukumbi wa Element uliopo Masaki jijini Dar es Salaam, Diamond alisema
kufuatia matusi hayo hatarajii kufika kwenye vikao vya usuluhishi na mtu
yeyote yule.
“Nimekasirishwa
sana na huyu jamaa (Prezzo) amenitukana kwenye mtandao mimi na demu
wangu (Wema) huku akijua sijawahi hata siku moja kujihusisha na yeye kwa
jambo lolote lile, daa!” alihamaki Diamond.
HASIRA ZOTE HIZO ZIMETOKA WAPI?
Diamond
aliyasema hayo baada ya meneja wa Prezzo aliyejulikana kwa jina moja la
Asa kumtaka Mbongo Fleva huyo wakutane yeye akiwa na Prezzo ili
wamalize tofauti zao.
“Meneja
wake aliniita eti tukakae kikao kuyaongea, mimi sioni sababu ya
kukutana na Prezzo, yeye ndiye alianza kunitukana hivyo kama anataka
kweli kuelewana na mimi basi arejee tena mtandaoni akaombe radhi,
nitamuona muungwana.
“Unajua
katika muziki ni wachache sana wenye uwezo wa kutumia ustaarabu katika
maamuzi yao, wengi wanaamini kumtusi mtu ndiyo njia pekee ya kupandisha
jina au kumfanya abusti ngoma yake kumbe huwa ni njia mojawapo ya
kujishushia heshima hasa kwa watu wenye busara walio nyuma yake.”
Mkali wa muziki kutoka Kenya, CMB Prezzo.
ANACHOKIAMINI DIAMOND
Akiendelea kuzungumzia ishu hiyo, Diamond alisema anachoamini yeye, Prezzo alifanya vile ili apate kiki kupitia mgongo wake.
“Najua
kama alifanya hayo kwa kufurahisha nafsi yake basi ilisuuzika.
Anachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kurudi mtandaoni akaandike mazuri
yangu.
“Kwanza mimi sina hata chembe moja ya chuki na yeye ingawa amenioneshea uswahili wa hali ya juu,” alisema Diamond.
WAKUTANA, WAFUNGIANA VIOO
Hivi
karibuni, wawili hao walikutana katika Ukumbi wa Element, Masaki, Dar
ambapo Prezzo alikuwa akifanya shoo lakini walifungiana vioo.
TURUDI NYUMA
Siku
za nyuma, iliwahi kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari vya
Tanzania na Kenya (hasa magazeti) kuhusu kuwepo kwa uhusiano wa
kimapenzi kati ya Wema na Prezzo ambao ulidumu kwa muda mfupi baada ya
Wema kumwagana na Diamond.Chanzo GPL
No comments :
Post a Comment