Stori: Mwandishi Wetu
KIMENUKA! Komediani aliyebahatika kuwa maarufu Bongo, Mujuni Silvery 'Mpoki' yuko
njiani kupandishwa kizimbani kufuatia mastaa waliodai aliwadhalilisha
usiku wa Tuzo za Kili kucharuka na kwenda kwa mwanasheria wao, Ijumaa
Wikienda lina ishu nzima.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, mastaa wanaodaiwa kutinga kwa mwanasheria na
kuandikisha maelezo ni hawa wafuatao: Mkurugenzi wa Aset Club
inayomiliki Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka,
mtangazaji wa runinga, Maimartha Jesse, Meneja wa Wema Sepetu, Martin
Kadinda na staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Wengine
ni Mbongo Fleva na mtangazaji, Vanessa Mdee, Miss Tanzania 2006, Wema
Sepetu, Aisha Ramadhani ‘Mashauzi’, Maria Sarungi na DJ Bonny Love.
WADAI KUDHALILISHWA BILA KUPEWA NAFASI
Chanzo
kilisema kwamba siku ya Tuzo za Kili, Mpoki akiwa MC wa shughuli hiyo,
aliwadhalilisha kwa kutangaza ndani ya hadhara iliyohudhuria kwenye
Ukumbi wa Mlimani City, Dar, mambo ambayo wenyewe hawakupata nafasi ya
kujitetea (balansi).
“Kule
kwa mwanasheria wao, wote walidai kuwa, siku ile Mlimani City, Mpoki
alikuwa akitangaza mambo yao, mengine ya siri, mengine si ya kweli,
mengine ya udhalilishaji bila wao kupewa nafasi ya kujitetea kama
mnavyofanya magazetini.
“Wenyewe
wanajua Mpoki hakutumwa na Kili kusema maneno yale bali aliamua yeye
kama yeye tu. Ndiyo maana wameamua kushughulika na Mpoki na si
mwingine,” kilisema chanzo hicho.
MADAI YAO YA MSINGI
Chanzo
kiliendelea kutiririka kwamba madai ya msingi ya mastaa hao kisheria
ni kudhalilishwa, kuzushiwa na kuchafuliwa mbele za watu, jambo ambalo
liliwapa usumbufu mbele za jamaa zao, wakiwemo watoto na ndugu wengine
waliokuwa wakifuatilia sherehe za utoaji wa tuzo hizo kubwa kuliko zote
Afrika Mashariki.
KASHFA ZENYEWE KWA UFUPI
Ili gazeti hili lisijiingize kwenye malalamiko ya mastaa hao linayaandika maneno hayo kwa ufupi sana lakini yenye kueleweka.
MAI; aliambiwa amezipiga jeki nido ilhali ana mtoto.
ASHA;
aliambiwa kwa usiku huo alipendeza sana (make up) lakini akionekana
kesho yake anaweza kupewa shikamoo kwa mabadiliko ya mwonekano.
RAY;
aliambiwa siku hizi amebadilika rangi, si kama zamani. Pia Mpoki
alimwambia amesikia ameachana na Johari na yuko na Chuchu Hans.
KADINDA; alimwambia anamuona anakwenda kumpa tuzo shemeji yake (Diamond)...
WEMA; alimuuliza ni kwa nini kila siku kwenye Instagram anatupia picha akiwa anakula mayai tu, anataka watu wamwelewe vipi!
VANESSA; alimwambia afanye mazoezi ya kutembela viatu vyenye visigino (na mengine ambayo si vyema kuyaandika hapa).
WIKIENDA LAWASAKA
Baada ya madai hayo, gazeti hili liliwasaka mastaa hao mmojammoja ili kusikia ukweli wa madai hayo.
Ijumaa Wikienda lilianza kwa kumsaka Kadinda juzi ambapo simu yake haikuwa ikipatikana hewani kama alivyozoeleka.
Kwa upande wake Ray alikiri kuwepo kwa uwezekano wa kumshitaki kwa kuwa ni kweli alimdhalilisha mbele ya kadamnasi.
Naye Mai alipotafutwa aliwaka akidai kuwa alichokifanya Mpoki hakikuwa sahihi kisheria hivyo jambo hilo lipo.
Kwa
upande wake, Isha Mashauzi alisema kuwa labda wenzake wameamua kumshtaki
Mpoki lakini hawakuwa wamemjulisha. Mastaa wengine ambao simu zao
ziliita bila kupokelewa ni Asha Baraka, Vanessa, Wema na DJ Bonny Love.
MSIKIE MPOKI
Mpoki
alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu malalamiko ya mastaa hao, katika
hali ya kushangaza alisema hakumbuki nini kilitokea siku hiyo.
“Kusema
ule ukweli mimi sikumbuki chochote kile kilichotokea siku ile, we
nitajie majina ya hao watu niwapigie halafu baadaye ndiyo tutaongea,”
alisema Mpoki akiweka sharti hilo wakati yeye ndiye aliyekuwa akiwananga
jukwaani.
ATUMA MESEJI YA HASARA!
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, Mpoki baada ya kupigiwa simu saa saba
alasiri na kujibu hivyo, usiku wa saa mbili alituma meseji kwa mwandishi
iliyosomeka:
“Hapo
ndipo uwezo wako wa kufikiri ulipoishia? Sijui lini mtafika kikomo cha
kuwa watumwa wa ujinga… Nisichokijua hakiwezi kunisumbua...”
AKIKUTWA NA HATIA KISHERIA
Kwa
mujibu wa mwanasheria mmoja (jina tunalo) aliyezungumza nasi, endapo
Mpoki akipanda mahakamani na kukutwa na hatia, anaweza kufungwa kifungo
cha miaka 5 jela au faini kulingana na uzito wa udhalilishaji huo kwa
mujibu wa walalamikaji.CHANZO GPL
No comments :
Post a Comment