Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, December 27, 2009

MSONDO NA "HUNA SHUKURANI" MIKOANI MWAKA MPYA

BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini Msondo Music bandi watafanya ziara ya utambulisho wa albam yao mpya ya huna shukrani ambapo Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kwamba Bendi hiyo kwa sasa ipo mikoa ya kusini kuwapa wapenzi burudani katika kutakiana heri ya mwaka mpya
Alisema katika utambulisho huo kwa mashabiki wa Msondo pia watapata nyimbo mpya kabisa zilizotungwa kwa ajiri ya albam ya mwaka 2010
Akielezea maandalizi zaidi Mhamila alisema licha ya kutambulisha albam bendi hiyo pia wamejipanga kutoa zawadi kwa mashabiki wao, ambapo albam yao mpya,iliyoingia sokoni hivi karibuni kuuzwa mtaani pia wameombwa kununuwa albam hiyo wapate kusikiliza majumbani mwao kwa ajiri ya sikukuu katika ziara hiyo ya utambulisho wa albamu siku ya alhamisi watakuwa Lindi katika ukumbi wa Comit Center, ijumaa Mtwara watapiga katika ukumbi wa Jakaya aidha jumamosi watapiga Masasi katika ukumbi maarufu na jumamosi watakuwa nachingwea katika ukumbi wa nachngwea pub, katika mkesha wa mwaka mpya watakuwa Rwangwa.
Alisema nyimbo zitakazotambulishwa katika dhihara hiyo ni pamoja na wimbo uliobeba albam hiyo, Huna shukrani uliotungwa na Saidi Mabera,Kiapo (husein jumbe) aki yangu ipo wapi (Uluka Uvuluge) Mama Cos, uliotungwa na marehemu (Josephe Maina) Albino (Juma Katundu) Machimbo Isihaka Kitima dj papa upanga) na Cheo ni Dhamana (Eddo Sanga)
Aidha aliwataja wanenguaji watakaokuwa wanatoa burudani katika safu hiyo kuwa ni Amina Said 'quen Emmy' Nacho Mpendu 'mama Nzawisa' na Amiri Saidi 'Dongo' aidha rapa wa bendi hiyo Romani Mng'ande 'Romario' atawachenguwa mashabiki watakaofika katika onesho hilo wakiongonzwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Muhidini Gurumo,na kiongozi wa bendi hiyo Saidi Mabela

No comments :

Post a Comment