Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, December 30, 2009

TWENDENI TUKAISHANGILIE STARS

Watanzania wametakiwa kuiunga mkono Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika mchezo wake wa kirafiki na Ivory Coast hapo Januari 4 utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam majira ya saa moja na nusu usiku.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka la Tanzania Fredrick Mwakalebela amesema timu ya Ivory Coast itawasili Jumamosi ya wiki hii ikiwa na msafara wa watu hamsini na watafikia hotel ya Kempisk.
Amesema Ivory Coast itacheza michezo miwili mmoja na Taifa Stars Januari 4 na mchezo mwingine itacheza na Timu ya Taifa ya Rwanda Januari 7 kwenye uwanja wa Taifa.
Akitaja viingilio vya mchezo huo Mwakalebela amesema viingilio vitakuwa ni vya aina saba tofauti, ambavyo ni Kijani mzunguko sh 5000, Bluu Mzunguko sh7000, Rangi ya Chungwa nyuma ya magori 10,000.
Rangi ya Chungwa mkabala na jukwaa kuu sh 20,000,
Viti maalum VIP C 30,000
Viti maalum VIP B 40,000
Viti maalum VIP A 50,000

No comments :

Post a Comment