Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, December 24, 2009

ZAIN SARAKASI KUWAPA BURUDANI ARUSHA X-MASS

MAONESHO ya Sarakasi yajulikanayo kama zain Sarakasi mama Afrika Mkoani Arusha watapata burudani katika kusherehekea sikukuu ya X-Mass na Mwaka mpya katika viwanja vya AICC vilivyopo Kijenge mjini Arusha.
Maonesho hayo yameandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain ikiwa ni mara ya pili kufanyika ambapo awali yalifanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana huku yakishirikisha wanamichezo wa mchezo huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja masoko wa Zain Costantine Magavilla alisema, maonesho hayo yatakuwa ni ya wiki mbili mfululizo ambapo yakiwa yameboreshwa zaidi ili kuweza kutoa burudani ya uhakika kwa watazamaji."Maonesho ya mwaka huu tumeyaboresha zaidi na yatazidi kuwa bora zaidi kadri miaka inavyokwenda ", alisema Magavilla.
Magavilla alisema, maonesho hayo ni maalum kwa ajili ya kusheherekea sikukuu za Krismas na mwaka mpya ambapo wakazi wa Arusha watafurahia shamrashamra hizo.
Alisema sambamba na maonesho hayo pia watachezesha droo kutoka kwenye majina na kadi za biashara watakazo kuwa wakiacha wateja pale wanapoingia kushuhudia maonyesho hayo.
Alisema washindi katika droo hiyo watajipatia vifurushi vya Zain vya huduma ya intaneti, kila siku hadi mwisho wa maonesho hayo.

No comments :

Post a Comment