Na Mwandishi
Wetu
SHINDANO la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' limepangwa kufanyika ifikapo June 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigamboni hapa jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu (pichani) alisema kuwa
maandalizi ya kinyang'anyiro hicho yanaendelea na warembo wenye sifa
kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanaombwa kujitokeza kushiriki.SHINDANO la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' limepangwa kufanyika ifikapo June 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigamboni hapa jijini Dar es Salaam.
Mratibu huyo kutoka kampuni ya K& L, alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa bora na kuwapa washiriki watakaokwenda kutwaa taji la Kanda ya Temeke na hatimaye taji la taifa la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
"Tumeshaanza mchakato wa shindano hili ambalo mwaka huu litakuwa na hadhi ya jiji la Kigamboni, tunawaomba wadau kushiriki kusaidia shindano hili liweze kufanikiwa," alisema Somoe.
Aliongeza kuwa mpaka sasa zaidi ya warembo 12 wameshajiandikisha kuwania taji hilo na wakiwa kambini watakuwa chini ya Hawa Ismail ambaye alikuwa mshindi ya shindano la Kanda ya Temeke mwaka 2003.
Alisema kuwa mazoezi ya shindano hilo yatakuwa yakifanyika kwenye ukumbi wa Brake Point iliyopo Posta jijini ili kutoa nafasi kwa washiriki kuweza kuhudhuria mazoezi hayo.
"Kigamboni ni zaidi ya kitongoji, tunaamini shindano letu litakuwa na mvuto na hadhi ya kipekee kama eneo lake lilivyo," aliongeza.
Alisema kuwa warembo watakaofanya vizuri watapata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika mashindano ya kanda ambayo yatafanyika baadaye mwaka huu.
Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine na NSSF.
Salha Israel kutoka Kanda ya Ilala ndiye mrembo anayeshikilia taji la taifa ambapo mwaka huu ratiba ya mashindano hayo imebadilika.
No comments :
Post a Comment