Kopo jipya la Castle Lite linavyoonekana sasa
Bia
maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) leo imezindua rasmi muonekano wa kopo lililojazwa
kinywaji hicho ikiwa ni muendelezo wa kuwarahisishia walaji upatikanaji
wa Bia hiyo iliyotokea kupendwa na watumiaji wa vileo na kuifanya iwe
bia inayokua kwa kasi hapa nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Castle
Lite Bi. Pamela Kikuli alisema; Leo tunazindua ujazo mpya wa bia ya
Castle lite, bia yenu muipendayo kwa sasa inapatikana katika kopo lenye
ujazo wa mililita 330. Uamuzi huu unatokana na mahitaji makubwa toka
kwa watumiaji na wapenzi wa bia hii ambayo imekuwa ikipatikana katika
chupa yenye ujazo wa mililita 375.
Wateja
wetu walihitaji kuipata bia yao popote pale walipo au kuwa nayo popote
waendapo, hivyo kupatikana kwa bia hii katika chupa peke yake
kulipunguza uhuru wa kuwa na bia yao popote waendapo kwani walihitaji
kurudisha chupa kila waitumiapo.
Uzinduzi
wa Castle lite ya kopo utasaidia zaidi kuongeza upatikanaji wa
kinywaji hiki katika maduka ya reja reja (super markets) n.k kote
nchini na kuwapa nafasi wapenzi wa castle lite kununua bia yao
waipendayo na kwenda nayo nyumbani. Bei ya reja reja kwa kopo ni
shilingi 1700/- na bei ya reja reja kwa chupa itaendelea kubaki ile ile
1700/-.
Kwa
upande wake Meneja mawasiliano na mahusiano ya jamii wa Tbl Edith
Mushi aliwashukuru wapenzi na watumiaji wa bia ya Castle Lite kwa
kuweza kuipa mafanikio makubwa katika soko la bia hapa nchini,
“ninawahakikishia kuwa mnafanya uamuzi ulio sahihi kwa kuchagua kutumia
Castle Lite” nasi tutaendelea kuwapatia bia iliyo bora siku zote.
Alisema Edith.
You might also like:
No comments :
Post a Comment