Mwakilishi
wa kampuni ya bia ya Serengeti Mkoani Iringa Bw. Philip Ghucha (kulia) akikabidhi
jenereta kwa mshindi wa promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO Bw.
Reymond Denis kutoka Iringa aliyejishindia jenereta hiyo kupitia bia ya Tusker
Lager, promosheni hiyo inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti nchi
nzima kwa wiki 16 kupitia bia za Premium Serengeti Lager,Tusker Lager na
Pilsner Lager ambapo zaidi ya milioni 180 zinashindaniwa
Mshindi wa jenereta Bw. Reymond
Denis(katikati) akielezea hisia zake baada ya kukabidhiwa jenereta ambapo
alisema kuwa hakutegemea kuwa atashinda lakini sasa anaamini kujaribu ni
kushinda na sasa anaweza kufanya kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia genereta
hiyo,” naishukuru sana SBL kwa kubadisha maisha yangu na kuwa bora zaidi.
Washabiki na wapenzi wa bia za
(SBL) wanywaji wa bia za Tusker na Serengeti wakimpongeza Bw. Reymond Denis ambapo baadaye
kila mmoja alipata nafasi ya kutoa maoni na kusema kuwa siku zote waliamini
promosheni ni uzushi lakini sasa wamejawa na imani, morali na hamu ya kuendelea
kushiriki, “ Kwanza tumefurahi sana SBL kutufuata hadi huku kijijini
kwetu kutuletea zawadi kwani tumezoea kampuni zingine wanakuita uifuate mwenyewe na
wakati mwingine mtu huna hata shilingi moja ya kusafiri wala ya kusafirishia
zawadi hiyo, tunawashukuru sana SBL.
No comments :
Post a Comment