23 Mei, 2012, Dar es Salaam. Tigo
imetangaza uzinduzi wa promosheni inayoipa pesa yako thamani, ijulikanao kama
‘Xtreme Pack’, kwa ajili ya mawasiliano ya jumla, yanayopatikana muda wowote na
wakati wowote.
Kwa kupiga
*148*01# au kutuma neno XTREME kwenda namba 15509, wateja wa huduma ya kulipia
kabla watafurahia huduma za thamani ambazo ni pamoja na dakika 15 za muda wa
maongezi zitakazowawezesha kupiga simu Tigo kwa Tigo, sms 100, 50 MB kwa ajili
ya kuperuzi facebook, kutumia mtandao, E-mail pamoja na Twitter, vyote hivyo kwa
gharama ya Tsh 450 na kuokoa Tsh 4,600! Pia tigo itatuma ujumbe mfupi wa maneno bure
kwa wateja wao, kuwataarifu juu ya ukomo wa matumizi ya vifurushi vyao na
kuwaruhusu kujiunga tena kama watahitaji .
“Tunatafuta
njia thabiti ya kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma zinazoendana na
thamani ya pesa zao” alisema Alice Maro ambaye ni afisa uhusiano wa Tigo. “Kwa kupitia
promosheni hii mpya wateja wataweza kutumia huduma za kusisimua kutoka simu za
apps, ambazo huduma na maudhui yake huboresha maisha, kazi na starehe zao.
Kuridhika kwa mteja ni kitu cha muhimu sana katika biashara yetu, na ndio maana
tunahakikisha kuwa tunabuni huduma na bidhaa zinazoridhisha na kuendana na
matakwa ya mteja,” alisema.
Tigo imeanzisha promosheni za kuaminika na zenye
uwazi kwa kufanya mawasiliano kuwa sio rahisi tuu kutumia bali zenye
thamani.
Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao wa simu za mkononi wa
kwanza Tanzania, ulianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania
wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini unaotoa huduma
katika mikoa 26, Tanzania Bara na Zanzibar.
Tigo ni sehemu ya Millicom
International Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama
nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni
43 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.
No comments :
Post a Comment