Dada Jestina George na dada Rahma Lupatu, wakijivunia Utanzania wao katika sherehe hizo za siku ya Afrika, zilizofanyika jana, Jijini London Uingereza.
Mheshimiwa Balozi wa Uganda, Mama Joan Rwabyomere, akifungua Maadhimisho ya siku ya Afrika nchini Uingereza, katika sherehe ambazozilifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lagham Palace, London.
Mheshimiwa Balozi wa Botswana, Bwana Roy Blackbeard, akihutubia katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika.
Kutoka
kulia, Dada Rahma Lupatu, Caroline Chipeta, Bwana David Nginila, Bwana
Kiondo (maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, London) na Dada Jestina George,
maarufu kama Queen wa Blog Uingereza.
Mabalozi ,Maafisa wa Ubalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wageni waalikwa katika sherehe hizo.
Kikundi cha ngoma kutoka Ghana, wakitoa burudani katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika hapa London.
***********************************
Siku
ya Afrika iliadhimisha rasmi jana hapa nchini Uingereza kwa kujuisha
nchi zote za Afrika zenye Balozi au Wawakilishi wao hapa nchini
Uingereza. Katika sherehe hiyo rasmi ya kuadhimishwa kwa Siku ya Afrika,
kulitolewa hotuba na Balozi wa Botswana na mbaye ni Mkuu wa Mabalozi wa
nchi za Afrika hapa Uingereza, Mheshimiwa Roy Warren Blackbeard.
Aidha Mheshimiwa Balozi Roy Blackbeard, alitoa salamu maalum kutoka kwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa nchi za Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, ambaye pia ni Raisi wa Benin.
Balozi
Roy, alielezea changamoto nyingi zinazo tokea Barani Afrika na
kwingineko na juhudi maalum zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa nchi za
Afrika kutatua migogoro na matatizo ya mara kwa mara yanayolikumba Bara
letu la Afrika.
Kabla
ya kutolewa hotuba hiyo, Balozi wa Uganda Mheshimiwa Mama Joan
Rwabyomere, alifungua kwa kuwakaribisha Mabalozi, Wawakilishi, Marafiki
wa Afrika na Wageni mbalimbali waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao
na kujumuika pamoja na waafrika wote duniani kuadhimisha siku hiyo hapa
nchini Uingereza.
Amani, Upendo, Ushirikiano na Mshikamano miongoni mwa nchi za Afrika vilihimizwa katika maadhimisho hayo.
No comments :
Post a Comment