Mnenguaji
mahiri wa bendi ya Mashujaa, Lilian Tungaraza ‘Internet’ akiongoza
kundi la wanamuziki wa bendi hiyo kulishambulia jukwaa wakati wa
uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki.
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akikabidhi
zawadi ya simu kwa, Baltazar Theobald, mshindi wa kwanza aliyeweza
kueleza vizuri jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa
5 wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa
wiki. Airtel Jiunge na Supa 5 Ilizinduliwa kwa mara ya kwanza jijini
Dar es Salaam hivi karibuni.
Wasanii
wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la Wanaume Family, Said Juma ‘Chege’
(kushoto) na Amani James Temba ‘Mheshimiwa Temba’wakionyesha makali yao
katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini
Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mpiga
tumba mahiri wa bendi ya Mashujaa Musica aliyejiunga na bendi hiyo
akitokea Twanga Pepeta, Sudi Mohamed ‘MCD’ akionyesha makali yake wakati
wa onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini
Dodoma mwishoni mwa wiki.
Rais
wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Cyprian ‘ Chaz Baba’
ambaye naye amehama akitokea Twanga Pepeta, akiimba wakati wa onyesho la
uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki.
Msanii
wa kundi la muziki wa bongo fleva la Tip Top Connection lenye maskani
yake mitaa ya Manzese jijini Dar es Salaam Hamad Ally ‘Madee’ akichengua
mashabiki wake waliojitokeza katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya
Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Huduma
ya SUPA 5 imepokelewa kwa shangwe mkoani Dodoma huku dhamira yake
ikiendelea kutimia baada ya umati mkubwa wa vijana kujitokeza ili
kufahamu vyema huduma hiyo nafuu iliyozinduliwa wiki moja iliypota kwa
lengo la kuwapa unafuu wateja wa Airtel ili kufurahia huduma tano nafuu
Wakati
wa uzinduzi huo uliofanyika katika tamasha la wazi katika viwanja vya
Barafu mjini Dodoma wasanii wa muziki wa Dansi na Bongo Flaver
walitumbuiza na kufanya tamasha hilo kufana zaidi
Miongoni
mwa wasanii waliotumbuiza kwenye utambilisho wa huduma hiyo mpya
kabambe ni pamoja na bendi ya muziki ya mashujaa, kundi la muziki wa
kizazi kipya la Tiptop Connection na kundi la Wanaume TMK.
Akitambilisha
huduma hiyo mbele ya wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake Meneja
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema, wateja wa kampuni hiyo
watapata unafuu mkubwa wa gharama za kupiga simu
“Huduma
ya SUPA 5 inamuwezesha mteja wa Airtel kutumia mtandao wa facebook bure
masaa 24, kuongea nusu shilingi na watu watatu, kupiga simu kwa robo
shilingi kuanzia saa 4 usiku hadi saa 12 asubuhi na kutumia huduma ya
internet bure usiku kucha” alieleza Bw, Mmbando
Huduma
ya SUPA 5 itaendelewa kutambulishwa katika mikoa mbali mbali kwa kuwa
huduma hiyo nafuu ni ya kudumu, mikoa inayotarajiwa kutembelewa kwa
kufanyiwa utambulisho rasmi wa huduma hiyo ya Airtel Supa 5 ni pamoja na
Morogoro, Iringa, Arusha, Mwanza na DSM.
No comments :
Post a Comment