Mbunge
wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan, akimvisha mkanda wa Ubingwa Taifa
(TPBO) Bondia Ramadhan Kumbele kutoka TMK, baada ya kumchapa mpinzani
wake James Mokiwa wa Kinondoni, katika pambano lao la Raundi 10, ambalo
lilimalizika katika raundi ya pili tu ya mchezo lililofanyika katika
ukumbi wa Vijana Kinondoni jana. Kumbele alishinda kwa KO katika raundi
ya pili.
Mbunge
wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan, akimwinua mkono juu Ramadhan Kumbele
kutoka TMK, baada ya kumchapa mpinzani wake James Mokiwa wa Kinondoni,
katika pambano lao la Raundi 10, ambalo lilimalizika katika raundi ya
pili tu ya mchezo lililofanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jana.
Kumbele alishinda kwa KO katika raundi ya pili.
Ramadhan
Kumbele, akimpeleka chini mpinzani wake James Mokiwa katika raundi ya
pili, Konde ambalo lilimfanya kushindwa kurejea na kuendelea na mchezo.
Mwamuzi
akimwesabia Bondia James Mokiwa bila mafanikio, kwani Bondia huyo
hakuweza kuinuka ili kuendelea na mchezo, jambo lililomfanya mwamuzi
huyo kumpatia ushindi Kumbele.
Bondia Swedy Hassan (kushoto) akichapana na mpinzani wake, Mwaite Juma, katika pambano hilo, Swedy alishinda kwa KO,
Doi Miyeyusho, (kulia) akimwadhibu mpinzani wake, Jumanne Mtengela. Katika pambano hilo, Doi alishinda kwa TKO.
Watoto, Martin Richard na Yohana Thomas, wakionyeshana umwamba katika mapambano ya utangulizi.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Singida, Chungai, akitoa burudani jukwaani.
No comments :
Post a Comment