Timu
ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Twiga Stars) inayotarajia
kuondoka leo saa 11.05 jioni kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwenda
Ethiopia imekabidhiwa Bendera ya Taifa na Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.
Twiga
Stars yenye msafara wa watu 24 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na
viongozi itacheza na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili
ya michuano ya mchujo kwa ajili ya Fainali za Nane za Kombe la Afrika
kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu Equatorial Guinea.
Mechi
hiyo itafanyika Mei 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa Addis Ababa wakati
ile ya marudiano itachezwa Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam. Twiga Stars ikifanikiwa kuitoa Ethiopia itakuwa imepeta
tiketi ya kwenda Equatorial Guinea.
Wachezaji
walioondoka na kikosi hicho ni Amina Ally, Asha Rashid (nahodha), Ester
Chabruma, Ettoe Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fadhila Hamad, Fatuma Bashiri,
Fatuma Khatib, Fatuma Mustafa, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma
Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Tamba, Mwapewa Mtumwa, Rukia
Hamis, Semeni Abeid na Zena Khamis.
Kwa
upande wa Benchi la Ufundi ni Charles Mkwasa (Kocha Mkuu), Nasra
Mohamed (Kocha Msaidizi), Furaha Francis (Meneja wa Timu), Mwanahamisi
Abdallah (Mtunza Vifaa) na Christina Luambano (Daktari wa Timu).
Twiga
Stars ambayo msafara wake unaongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira
wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itarejea
nyumbani Mei 28 mwaka huu saa 6 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
No comments :
Post a Comment