Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akimkabidhi Bendera ya Taifa
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Twiga Stars wakati wa hafla
ya kuiaga timu hiyo inayokwenda Addis Ababa Ethiopia kwenye mashindano
ya soka ya Kombe la mabingwa wa Afrika kwa upande wa wanawake.Kushoto
kwa Waziri ni Kaimu Mkurugenzi wa TFF Bw. Sanday Kayuni.( Picha na Benjamin
Sawe wa WHVUM)
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akimkabidhi Meneja wa Timu
ya Wanawake Twiga Stars Furaha Francis kitita cha Dola za Kimarekani
3500 kama mchango wa Serikali kw timu hiyo inayokwenda Addis Ababa Ethiopia
kwenye mashindano ya soka ya Kombe la mabingwa wa Afrika kwa upande
wa wanawake.Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa TFF Bw. Sanday
Kayuni. ( Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Twiga Stars) inayotarajia kuondoka leo saa 11.05 jioni kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwenda Ethiopia imekabidhiwa Bendera ya Taifa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Twiga Stars) inayotarajia kuondoka leo saa 11.05 jioni kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwenda Ethiopia imekabidhiwa Bendera ya Taifa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.
Twiga
Stars yenye msafara wa watu 24 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na
viongozi itacheza na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili
ya michuano ya mchujo kwa ajili ya Fainali za Nane za Kombe la Afrika
kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu Equatorial Guinea.
Mechi
hiyo itafanyika Mei 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa Addis Ababa wakati
ile ya marudiano itachezwa Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam. Twiga Stars ikifanikiwa kuitoa Ethiopia itakuwa imepeta
tiketi ya kwenda Equatorial Guinea.
Wachezaji
walioondoka na kikosi hicho ni Amina Ally, Asha Rashid (nahodha), Ester
Chabruma, Ettoe Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fadhila Hamad, Fatuma Bashiri,
Fatuma Khatib, Fatuma Mustafa, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma
Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Tamba, Mwapewa Mtumwa, Rukia
Hamis, Semeni Abeid na Zena Khamis.
Kwa
upande wa Benchi la Ufundi ni Charles Mkwasa (Kocha Mkuu), Nasra
Mohamed (Kocha Msaidizi), Furaha Francis (Meneja wa Timu), Mwanahamisi
Abdallah (Mtunza Vifaa) na Christina Luambano (Daktari wa Timu).
Twiga
Stars ambayo msafara wake unaongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira
wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itarejea
nyumbani Mei 28 mwaka huu saa 6 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
LIGI YA TAIFA KUANZA MEI 27
Ligi
ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa sasa itaanza Mei 27 mwaka
huu badala ya Mei 26 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali. Uamuzi
wa kusogeza mbele kwa siku kuanza kwa ligi hiyo uliofanywa na Kamati ya
Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana
jana (Mei 23 mwaka huu).
Timu
23 zitachuana katika kinyang’anyiro hicho kitakachofanyika katika vituo
vya Kigoma (Uwanja wa Lake Tanganyika), Musoma (Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume) na Mtwara (Uwanja wa Umoja) ambapo kinatarajia kumalizika Juni
13 mwaka huu.
Kituo
cha Kigoma kina timu za Aston Villa ya Singida, Bandari (Kagera), CDA
(Dodoma), JKT Kanembwa (Kigoma), Majimaji (Tabora), Mwadui (Shinyanga)
na Pamba (Mwanza).
Ashanti
United ya Ilala, Flamingo (Arusha), Forest (Kilimanjaro), Korogwe
United (Tanga), Nangwa VTC (Manyara), Polisi (Mara), Red Coast
(Kinondoni) na Tessema ya Temeke ziko kituo cha Musoma.
Kituo
cha Mtwara kina timu za Kurugenzi ya Iringa, Lindi SC (Lindi), Mighty
Elephant (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Mpanda Stars (Rukwa),
Ndanda (Mtwara), Super Star (Pwani) na Tenende (Mbeya).
MALAWI YATUA KUIVAA TAIFA STARS
Timu
ya Taifa ya Malawi (The Flames) inatarajiwa kuwasili nchini leo saa 10
jioni kwa ndege ya Air Malawi kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya
Taifa Stars itakayofanyika Jumamosi (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mechi
hiyo ni kwa ajili ya kuipima nguvu Taifa Stars kabla ya mechi yake
mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast
itakayofanyika Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan. Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini chini ya Kocha Kim Poulsen.
Malawi
itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu ambapo
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na
kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP B na C
wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
Malawi
ambayo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu
baada ya mechi hiyo itakwenda Zanzibar ambapo Mei 28 mwaka huu itacheza
na Zanzibar Heroes.
Makocha
wa timu zote mbili Taifa Stars na The Flames kesho (Mei 25 mwaka huu)
saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za
TFF.
No comments :
Post a Comment