Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya SBL, Teddy Mapunda akizungumza na
Waandishi wa Habari, City Sports Lounge asubuhi ya leo. Wengine kulia
ni Katibu Mkuu wa TASWA Amir Mhando na katikati ni Mwenyekiti wa TASWA,
Juma Pinto
|
SOURCE: FULL SHANGWE
KAMPUNI
ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL), imetangaza rasmi kudhamini kwa
kitita cha Sh. Milioni 150, tuzo za Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA), hafla ambayo inatarajiwa kufanyika mapema
mwezi ujao.
Tukio
hilo la kihistoria litafanyika katika ukumbi maarufu hapa jijini Dar es
Salaam Diamond Jubilee tarehe 14/06/2012 ambapo zaidi ya wageni 500
wanatarajiwa kufurika kushuhudia tukio hilo.
Akizungumza
katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es salaam leo asubuhi,
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda, amesema
maamuzi ya kudhamini tukio hilo kwa mara nyingine ni kuendelea kusaidia
kuinua michezo nchini.
“Kufanya hivi
ni sehemu mojawapo ya kuwatambua wanamichezo, lakini pia kupitia
udhamini huu, tungependa kuwasaidia waandishi wa michezo kujaribu
kuangalia ndani zaidi na kuleta mwanga na uelewa wa haraka kwa jamii
juu ya michezo mbalimbali iliyopo hasa hapa kwetu Tanzania”alisema
Mapunda.
Udhamini huu
utatumika katika maeneo mbalimbali kufanikisha sherehe hiyo kama vile
chakula cha jioni, burudani,tuzo, vyeti, zawadi pamoja na mahitaji na
matumizi mengine ili zoezi hili liwe nzuri na la kukumbukwa nchini”,
aliongeza Bi. Mapunda.
Mkurugenzi
huyo aliongeza kuwa kampuni ya bia ya Serengeti inajivunia kuwa
mdhamini mkuu wa tuzohizi kwa mwaka wa tatu sasa. “sisi kamaSBL
kwakweli tunajivunia kuwa wadau wa tukio hili kwa mara nyingine, lakini
pia tunajivunia kuwa na waandishi bora wahabari za michezo ambao
wamekuwa mstari wa mbele katika kuinua na kuendeleza tasnia ya michezo
hapa nchini kupitia taarifa sahihi zenye kuelimisha jamii juu ya swala
zima la michezo” .
SBL imekuwa
mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo hya michezo Tanzania na kwa
sababu hiyo, inachukuliwa kama kampuni mfano wa kuigwa
No comments :
Post a Comment