CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pongezi kwa
Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Tanzania Daima, Tullo Chambo
(pichani kushoto) kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Chama cha Riadha Tanzania (RT).
Katibu Mkuu wa TASWA, Amiri Mhando amesema
mchana huu kwamba, Chambo alitwaa nafasi hiyo kwenye Uchaguzi Mkuu wa
RT uliofanyika Jumapili mjini Morogoro, ambapo ni miongoni mwa wajumbe
wapya walioingia kwenye chama hicho.
Wengine walioshinda ni Anthony
Mtaka ambaye anakuwa Rais mpya wa RT, wakati Makamu wa Rais Utawala ni
William Kallaghe, Makamu wa Rais Ufundi, Dk. Ahmed Ndee, Katibu Mkuu,
Suleiman Nyambui, Katibu Msaidizi, Ombeni Zavalla, Mhazini, Is-Haq
Suleiman.
Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji ni Mwinga Mwanjala, Meta Petro, Peter Mwita,
Rehema Killo, Lwiza John, Zakaria Barrie, Zakaria Gwanda, Robert Kalyahe
na Christian Matembo.
TASWA
inatambua Chambo ni mwanahabari mzoefu, ambaye kwa muda mrefu amekuwa
mhariri wa habari za michezo na ni mtu mwenye kujua mambo mengi
yanayohusu riadha, hivyo atakuwa kiungo muhimu kwa watu wa riadha, pia
atakuwa kiongo kizuri kwa waandishi wa habari za michezo kuhusiana na
mambo ya riadha.
TASWA
inaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kadri itakavyoweza na inamtakia
kila la heri, huku ikiamini hatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa RT
waliomuamini wakamchagua kushika wadhifa huo.
Pia
Taswa inawapongeza viongozi wote wa RT walioingia madarakani Jumapili,
ikiamini watakuwa chachu ya mafanikio ya riadha hapa nchini.
No comments :
Post a Comment