Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akimkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo vibali vya ujenzi wa jengo hilo, kushoto ni Mwenyekiti wa Madhehebu ya Khoja Shia Shiraz Walji
--
MFANYABIASHARA
maarufu nchini, Mustafa Sabodo ametoa zaidi ya sh.bilioni 5 kwa
madhehebu ya Khoja Shia Ithnaashri Jamat kwa ajili ya kujenga jengo la
maegesho ya magari.
Akizungumza katika hafla ya kupokea vibali vya ujenzi wa jengo hilo
Dar es Salaam leo kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa
alisema jengo hilo litasimamiwa na madhehebu hayo.
Alisema jengo hilo lililopo katika mitaa ya India na Morogoro la
ghorofa 14 litakuwa na uwezo wa kuhifadhi magari 180 kwa wakati mmoja.
Silaa alisema fedha zitakazopatikana kwa malipo ya maegesho ya magari
katika kipindi cha miaka 10 zitafanya kazi ya kuchimba visima katika
maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Meya alisema kwa muda mrefu Jiji la Dar
es Salaam limekuwa likikabiliwa na maeneo ya kuegesha magari na kuwa
jengo hilo la kwanza kubwa litakuwa ni mkombozi mkubwa.
"Kwa muda mrefu tumekuwa na matatizo ya kuegesha magari katika jiji
letu hivyo msaada aliotoa ndugu yetu Sabodo kwa madhehebu hayo ya
ujenzi wa maegesho hayo itasaidia sana kupunguza tatizo hilo," alisema
Silaa.
Alisema Manispaa imepokea jambo hilo kwa mikono miwili na ndio maana
imekamilisha vibali ili ujenzi huo uende pasipo kikwazo chochote.
Alisema jengo hilo litaitwa Sabodo Car Park jambo litakalo weka
kumbukumbu ya mchango wake katika kufanikisha shughuliza za maendeleo.
Mwenyekiti wa Madhehebu hayo Shiraz Walji, alimshukuru Sabodo kwa
msaada wake huo na kuahidi kusimamia vizuri mradi huo ambao utakuwa wa
manufaa kwa Watanzania wote.
No comments :
Post a Comment