Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, April 3, 2010

SIMBA KURUDI DSM JMOS, KADUGUDA AJITOSA UCHAGUZI SIMBA


Wekundu wa Msimbazi Simba wanarejea Jumamosi kutoka kwenye marashi ya karafuu huko kisiwani Unguja Zanzibar wakisema wako tayari kupeperusha Bendera ya Tanzania hapo Jumapili kwenye mchezo wao wa marejeano kombe la shirikisho dhidi ya Lengthens ya Zimbabwe.

Meneja wa Simba Innocent Njovu amesema kikosi kiko vizuri licha ya kuwa majeruhi Kelvin Yondan Mbuyi na David Naftal Tevelu.

Wapinzani wa wekundu hao Lengthens waliokuwa watue Ijumaa sasa watatua Jumamosi jioni kwa ndege ya Kenya Airways KQ.

Kwenye gazeti la The HERALD la Zimbabwe nahodha wa kikosi hicho amesema wanafahamu kuwa Simba watatumia mbinu zote chafu wakati watakapofika lakini wachezaji wanafahamu na wanajiamini kuiondoa Simba nje ya michuano hiyo ingawa waliwafunga mabao 3-0 kwenye ardhi ya nyumbani kwao.

Sehemu ya taarifa hiyo inasomeka We are fully aware that Simba will Employ all dirty tactics as soon as we arrive but the players are oozing with confidence to knock out Simba on there home land despite having sufferd a big 3-0 on our home land
Wakati huohuo Ikiwa imeingia siku ya pili ya kuchukua fomu za kuwania ubosi ndani ya klabu ya Simba mwanachama maarufu na aliyewahi kuwa bosi wa Shirikisho la soka nchini TFF wakati huo ikifahamika kama FAT Alhaji Ismail Aden Rage naye leo amejitosa kuwania kuiongoza klabu hiyo.

Rage amechukua fomu ya kuwania nafasi ya mwenyekiti akiwa ni wa pili kwenye nafasi hiyo baada ya Mohamed Nanyali kufanya hivyo jana lakini akiwa mwanachama wa nne kufanya hivyo baada pia ya hapo jana Geofrey Nyange Kaburu na Mwina Mohamed Seif Kaduguda kufanya hivyo.

Nafasi zinazowaniwa ndani ya klabu hiyo ni Nafasi ya Mwenyekiti,makamu mwenyekiti na wajumbe saba wa kamati ya utendaji huku zile za juu zikilipiwa kwa kiasi cha shilingi laki 2 kila moja na zile za ujumbe zikilipiwa kwa kiasi cha shilingi laki 1.

Uchaguzi wa klabu hiyo unataraji kufanyika May 9 mwaka huu.

No comments :

Post a Comment