Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, April 13, 2010

YANGA WAIFUATA SIMBA ZANZIBAR

Watoto wa Jangwani Yanga siku ya Jumatatu wamekwea boti kuelekea kisiwani Unguja Zanzibar kumtembelea mama Karume huku wakiichukulia siku hiyo kama ya mapumziko.

Kocha wa Yanga MSerbia Kostadin Papic anasema safari hiyo ya Zanzibar ni moja ya maandalizi yao japo wengi wanaona ni kama mapumziko ya kutofanya mazoezi.

Papic anasema kwenda Zanzibar na kurejea kesho ni moja ya programme ya maandalizi yao huku akisema hata hivyo mchezo huo wa Jumapili hauna uzito mkubwa kwakuwa tayari Simba washatwaa uchampion huku Yanga ikiwa imeshakamata nafasi ya pili na matokeo yake hayatabadili lolote kwenye msimamo wa ligi.

Nahodha wa Yanga Abdi Kassim amesema kwao ni moja ya mapumziko lakini pia ni mazoezi kwao japo wako tayari kwa mchezo huo wa Jumapili dhidi ya mahasimu wao Simba.

Mahasimu wa Yanga katika soka, Wekundu wa Msimbazi Simba wao wamepiga kambi yao huko kisiwani Unguja Zanzibar kwaajili ya mchezo huo wa Jumapili.

No comments :

Post a Comment