Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, May 7, 2012

AIRTEL YASHIRIKI UWEKAJI WA MKONGO WA MAWASILIANO KUTOKA DAR-TANZANIA HADI NCHINI SHELISHELI (SEYCHELLES)



 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya akihojiwa na vyombo vya habari katika hafla ya uzinduzi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.
 Waziri wa Viwanda na Maliasili wa Seychelles, Peter Sinon (kushoto), wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia), mafundi na wawakilishi kutoka Seychelees na Tanzania wakionyesha kipande cha mkongo wa mawasiliano kama ishara ya uzinduzi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.


Katibu Mkuu Idara ya Mwasiliano na Teknolojia katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Seychelles, Benjamin Choppy (katikati) akihojiwa na vyombo vya habari katika hafla ya uzinduzi wa wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana.  Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.  Kushoto ni Mwakilishi wa kampuni ya Airtel nchini Seychelles, Gail Talma Jumeau na kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya.
---

Waziri wa Maliasili na Viwanda wa Shelisheli Bw. Peter Sinon amesema nchi yake itanufaika na upatikanaji wa mawasiliano ya mkongo wa taifa kutoka Tanzania kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya taifa hilo.
Mkongo wa taifa wa mawasiliano uliozinduliwa miaka 2 iliyopita na Rais Jakaya Kikwete umeweza kuzinufaisha nchi jirani kama Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi na sasa Shelisheli.
Akiongea katika fukwe za bahari ya hindi jijini Dar es Salaam eneo la msasani ambako uwekaji wa mlongo huo ndio ulikoanzia mwishoni mwa wiki hii Waziri Sinon amesema kuwa mpango huo ukimalika utaiweza nchi yake kukuza sekta ya mawasiliano na upatikanaji wa taarifa mbalimbali jambo litakalo saidia kukuza uchumi wa nchi hiyo.
“Hii ni nafasi nzuri ya kipekee na ndio maana hata sisi shelisheli tunaipa kipaumbele ili kukamilisha zoezi hili la uwekaji wa mkongo huu wa mawasiliano, tunaamini tukimaliza kila kitu itasaidia sana kukuza pato la nchi kulingana na umuhimu wa mawasiliano” alisema Bw Peter Sinon- Waziri wa Maliasili na Viwanda Shelisheli
Kwa uapnde wake Katibu Mkuu kiongozi kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT Bw Benjamin Choppy ameelezea faida za uwepo wa mkongo huo kuwa ni pamoja na kutoa mawasiliano ya uhakika na bora kwa nchi hiyo
“Sasa hii ni dalili ya kutoa bidhaa bora ya mawasiliano kwa kuwa ukamilifu wa uwekaji mkongo huu tutapata mwasiliano bora zaidi” alimaliza kwa kusema Katibu Mkuu kiongozi kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT Bw Benjamin Choppy
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano Mallya ameelezea upatikanaji wa teknolojia hiyo mpya ya mawasiliano kuwa ni kati ya vitu ambavyo Airtel inavifanyia kazi kuhakikisha inaunganisha mataifa mengi ili kutoa mawasiliano yanayotoa nafasi au fulsa ya kuendeleza nchi hizo kijamii na kiuchumi pia  
“Tunaamini ushirikiano wetu na wenzetu wa shelisheli ni dhahiri utachangia sana kuboresha mahusiano yetu kibiashara na pia kutoa nafasi kwa nchi hizi kujijenga kijamii ma kiuchumu kutokana na faida ya mahusiano haya ya kulaza mkongo huu wa kuunganisha mawasiliano” alisema Bi Beatrice Singano Mallya
Aitel Tanzania na Airtel Shelisheli kwa kushirikiana na SCS zinatekeleza mpango wa kuweka mkongo wa taifa kwa lengo la kuiwezesha nchi hiyo kuwa na mawasiliano ya uhakika.

No comments :

Post a Comment