Meneja wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akiongea na waandishi
wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua Hazina chini
ya Kizibo inayoendesha na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake
za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager, kulia ni Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa kampuni ya Serebgeti (SBL) Teddy Mapunda.
Meneja wa Bia ya Serengeti Premium Lager Allan Chonjo akiongea na
waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua
Hazina chini ya Kizibo inayoendesha na kampuni ya bia ya Serengeti
kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager,
kutoka kulia ni Meneja wa bia ya Tusker Ritah Mchaki, Mrisho kutoka
shirika la Bahati Nasibu ya Taifa na Teddy Mapunda mkurugenzi wa
Mawasiliano (SBL)
Droo ya kwanza kabisa ya promosheni inayoendelea ya kampuni ya bia
ya Serengeti Breweries LTD (SBL) inayojulikana kama‘Vumbua hazina
chini ya kizibo’ imefanyika leo katika ofisi za kampuni hiyo, maeneo
ya Oysterbay jijini Dar Es salaam.
Kampuni ya bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya kampuni ya DIAGEO
PLC (UK) ya Uingereza na kupitia bidhaa zake, Serengeti Premium Lager,
Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni hii tangu wiki iliyopita.
Promosheni hii ya aina yake iliyosheheni zawadi mbalimbali kubwa na
ndogo kama vile Jenereta , Pikipiki , Bajaji , Gari na zawadi zingine
nyingi zikiwemo pesa taslimu na bia za bure.
Droo hii leo, ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka
Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni
hii, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE na wahakiki
na wakaguzi kutoka PriceWaterHouseCoopers (PwC) kuonesha jinsi washindi
wote watapatikana kihalali.
Akiongea katika hafla hii, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager,
Bw. Allan Chonjo amesema kwamba “Tayari tumeweza kupata washindi waliopata
pesa taslimu na wakafanikiwa kupata pesa zao kupitia MPESA ndani ya
masaa 24. Pia, washindi wamepatikana ambao wamejishindia zawadi
za vinywaji vilivyopo katika promosheni hii. Naomba nisisitize,
kwamba promosheni hii inalenga kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania
hususani wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni yetu ikiwa ni sera
mojawapo ya kampuni hii kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia
bidhaa zake zenye ubora wa kipekee. Pia ningetaka niseme ni njia
ya pekee ya kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano wao kwetu”.
Mshindi wetu wa droo ya kwanza ni John Gati mwenye umri wa miaka thelathini
na mbili kutoka Musoma ambaye amejishindia jenereta pamoja na
Godfrey Shao mwenye umri wa miaka ishirini na nne kutoka Mwanza aliyejinyakulia
Bajaj. Baada ya kuchezeshwa droo kwa umakini kabisa na Rita Mchaki
-Meneja wa bia ya Tusker Lager alipiga simu kwa washindi na ilikuwa
dhahiri kwamba washindi walishtuka na kufurahia ushindi wao. Baada
ya maongezi machache, waliweza kujieleza vizuri majina yao kamili na
wanapopatikana ili waweze kupatikana siku chache zijazo kwenye hafla
fupi ya kuwakabidhi zawadi zao.
No comments :
Post a Comment