Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa kampuni ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza washindi wa
Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni ya bia
ya Serengeti kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na
Serengeti Lager.
Meneja
wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo (tatu kulia) akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua
Hazina chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti
kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager,
kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serebgeti (SBL) Teddy
Mapunda,pamoja na Bw. Bakari Maggid kutoka shirika la Bahati Nasibu ya
Taifa na kushoto ni muwakilishi kutoka kampuni ya PWC,Tumainiel Malisa
Meneja wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akizungumza na mmoja wa washindi kwa njia ya simu
Pichani
ni Wawakilishi kutoka kampuni ya Pricewaterhouse Coopers
(PWC),Tumainiel Malisa (shoto) na James Ndetiko (kulia) sambamba na Bw.
Bakari Maggid kutoka shirika la Bahati Nasibu ya Taifa wakifuatilia
kupatikana kwa washindi wawili wa bahati nasibu ya Promosheni Vumbua
Hazina chini ya Kizibo
*****
Ni katika droo ya promosheni ya ‘vumbua hazina chini ya kizibo ’
Mei
9, 2012 Dar Es Salaam: Droo ya pili ya Promosheni inayoendelea ya
kampuni ya bia ya Serengeti inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya
kizibo’ imefanyika leo katika ofisi za kampuni hiyo maeneo ya Oysterbay
jijini Dar Es salaam.
Kampuni
ya bia ya Serengeti kupitia bidhaa zake, Serengeti Premium Lager,
Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni nchi nzima
ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’
Promosheni
hii ya aina yake iliyosheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama
vile Jenereta (kangavuke), Pikipiki, Bajaji, Gari ndogo aina (saloon) na
zawadi zingine nyingi zikiwemo pesa taslimu. Katika promosheni hii
zawadi za thamani zaidi ya Tsh MILLIONI 780 kushindaniwa.
Droo
hiyo ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya
Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo,
wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na
wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers ili kuhakikisha washindi
wote wanapatikana kihalali.
Akiongea
waandishi wa habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa mahusiano na
mawasiliano wa kampuni ya SBL Bi. Teddy Mapunda amesema kwamba “Tayari
tuna washindi zaidi ya elfu moja mia tano, wamejishindia pesa taslimu na
kuzipata kupitia njia ya MPESA.
Hawa
washindi ni pamoja na wanaoshinda bidhaa zenyewe zilizoorodheshwa
katika promosheni hii. Vile vile, kama mlivyoshuhudia asubuhi ya leo,
tumepata washindi wawili wa jenerata, na sio mmoja kama ilivyo kawaida .
Hii ni kwa sababu katika promosheni hii, kuna vigezo na masharti
yanayozingatiwa”.
Masharti
ya promosheni hii tunayazingatia kweli kweli na kwa sababu hiyo,
mshindi wetu wa wiki iliyopita wa jenerata ilikuja kugundulika
hakustahili kushiriki katika promosheni hii. Tunataka kuwaeleza
watanzania kwamba hii promosheni ni ya uhakika na kwa kweli mnavyoona,
ina uangalizi mkubwa na inaendeshwa kwa umakini kabisa. Nawaomba wateja
wetu waendelee kushiriki ili waendelee kushinda.” Aliongeza mkurugenzi
huyo.
Washindi
katika droo ya leo waliojishindia jenereta ni Amadeus Minja mkazi wa
pugu na Agnes Msengi wote wakia ni wakazi wa jijini Dar Es Salaam na
Ibrahim Kimambo mkazi wa Tabata Kimanga jijini Dar Es Salaam
aliyejishindia Pikipiki .
Allan
Peter Chonjo, Meneja wa Bia ya Serengeti Premium Lager alipiga simu kwa
washindi na ilikuwa dhahiri kwamba washindi walishtuka na kufurahia
ushindi wao. Baada ya maongezi machache yaliyofanyika kwa njia ya simu
washindi hao waliweza kujieleza vizuri majina yao kamili na
wanapopatikana ili waweze kupatikana siku chache zijazo kwenye hafla
fupi ya kuwakabidhi zawadi zao.
No comments :
Post a Comment