Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, December 31, 2013

MABONDIA WATIFUANA USIKU WA KUINGIA MWAKA MPYA




Bondia Joshua Amukulu(kushotO) wa Kenya akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransis Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa kufunga mwaka na kukaribisha mwaka uliofanyika katika ukumbi wa msasani klabu Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya pili na kuibuka mbabe katika mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Joshua Amukulu(kushotO) wa Kenya akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransis Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa kufunga mwaka na kukaribisha mwaka uliofanyika katika ukumbi wa msasani klabu Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya pili na kuibuka mbabe katika mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana kakonde na Mustafa Dotto wakati wa mpambano wao wa raundi sita kwa ajili ya kufunga mwaka king class mawe alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mustafa Dotto kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao king class alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Mustafa Dotto kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao king class alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
USHINDI RAHA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AKINULIWA MKONO JUU BAADA YA KUMDUNDA MUSTAFA DOTTO WAKATI WA KUSHEREKEA USIKU WA MWAKA MPYA ZAIDI TEMBELEA www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Kalama Nyilawila kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makone na Ibrahimu Maokola wakati wa mpambano wao ulifanyika kwa ajili ya kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya Kalama  alishonda kwa k,o ya raundi ya pili  www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Iddy Mnyeke  kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao wa kuuwaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya mpambano huo ulito droo  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Cosmas Cheka na Iddy Mnyeke wakipambana

MABONDIA WAKISUBILI MATOKEO AMBAYO YALIKUWA NI DROO

Samsung Tanzania yapata Ongezeko la wateja Kusajili bidhaa kwa zaidi ya 30%


Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw Sylvester Manyara (kushoto) akimkabidhi funguo ya gari mshindi wa jumla wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Juma Musa Ramadhani mkazi wa Tabata Segerea jijini Dar es Salaam mara wakati wa hafla ya kukabidhi rasmi zawadi hiyo ya Mitsubishi Double Cabin, tukio linaloshuhudiwa kwa ukaribu na Msimamizi muandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bw. Bakari Maggid wa kwanza kulia.

EXTRA BONGO YAMREJESHA KUNDINI MASTER B ALIYEKUWA AMETIMKIA TWANGA





Mnenguaji wa kiume wa Extra Bongo, Master B, aliyekuwa ametimkia bendi ya Twanga Pepeta, wa kwanza (kushoto) akiwajibika na wenzake wakati wa moja ya onesho laeo kabla ya kuihama bendi hiyo, ambaye atatambulishwa rasmi kurejea kundini Extra Bongo.


Na Mwandishi Wetu
BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo ya jijini Dar es Salaam, imemrejesha kundini mnenguaji wake mahiri wa kiume Kassim
maarufu kwa jina la ‘Master B’.

Mnenguaji huyo alitimkia katika bendi ya Twanga pepeta ya jijini Dar es Salaam na kudai kuwa alirubuniwa kufanya hivyo.

Msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa alisema kuwa kuondoka kwa mnenguaji huyo kulifanya idadi ya wanenguaji wa kiume kupungua kutoka watano hadi wanne.

Naye Master B alikiri kurubuniwa na wadau wa Twanga Pepeta hadi kukubali kuhamia huko lakini alieleza kuwa alipofika huko maisha yalikuwa magumu tofauti na alivyotarajia baada kipindi chote alichokaa huko kushindwa kupewa mkataba tofauti na ilivyokuwa matarajio.



“Mimi nimeamua kurudi baada ya kuona mambo magumu Twanga Pepeta na mipango yangu haiendi sawa ,hivyo nimerudi katika bendi yangu ya nyumbani na naahidi nitafanya vyema kama ilivyokuwa hapo awali na kukosea kwa mwanadamu kumeumbwa,”alisema Master B.
Naye kiongozi wa wanenguaji Hassan Mussa maarufu kwa jina la ‘Super Nyamwela’alisema amempokea Master B baada ya kuomba radhi kwa kile alichokifanya na kuiahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kuimarisha safu ya unenguaji.
Alisema alipoondoka Master B kulibakiwa na wanenguaji wanne lakini kwa sasa kuna idadi ya waenguaji watano na kwamba hali imerudi kama ilivyokuwa awali.
Aliwataja wanenguaji wa kiume waliopo kwenye kikosi hiko uwa ni pamoja na Super Nyamwela mwenyewe,Danger boy,Dogo White, Ally Koncho na Master B.
Tayari Master B yupo Geita, Mwanza na Extra Bongo kwa ziara ya wiki moja moja ambapo leo watakuwa wakiukaribisha mwaka mpya wa 2014.

RAIS KIKWETE AMWAPISHA IGP MPYA PAMOJA NA NAIBU WAKE IKULU


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. PICHA NA IKULU

BREAKING NEWSsss TUMEVUKA MWAKA 2014 SALAMA







Viongozi  wa  wananchi wa mji  wa Iringa  wakiimba  wimbo wa taifa  la Tanzania  kuufurahia mwaka  2014  leo  uwanja wa Samora

MWAKA MPYA 2014 WAANZA KWA AJALI MBAYA IRINGA NI DAKIKA 20 BAADA YA MWAKA MPYA




Hii ni ajali mbaya ya  piki piki iliyotokea  eneo la  Ilala katika Manispaa ya  Iringa  ikiwa ni dakika 20 baada ya  kuaga mwaka  2013 na kuukaribisha  mwaka  2014 
Hawa ni majeruhi wa ajari hiyo kushoto ni dereva wa  boda boda JOseph Nyegele na kulia ni abiria  wake ambae hajitambui kabisa
Wasamaria  wema  wakisaidia  kushusha majeruhi ambao wamepata ajali ya pikipiki usiku  huu  wakati wakiuanga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014  leo mjini Iringa

Monday, December 30, 2013

MABONDIA WATAMBIANA KUMALIZA UBISHI DESEMBA 31 MSASANI KLABU





Bondia Joshua Amukulu kushoto kutoka Kenya akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho wakati wa upimaji uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Desemba 31 siku ya jumanne katika ukumbi wa Msasani klabu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Kalama Nyilawila kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Maokola  baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Desemba 31 siku ya jumanne katika ukumbi wa Msasani klabu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Miyeyusho akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake  Joshua Amukulu kutoka Kenya utakaofanyika Desemba 31 siku ya jumanne katika ukumbi wa Msasani klabu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO AKIOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE NA MKENYA JOSHUA AMULU UTAKAOFANYIKA DESEMBA 31 KATIKA UKUMBI WA MSASANI KLABU PICHA ZAIDI TEMBELEA www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ibrahimu Class 'king Class Mawe'  kushoto akitunishiana misuli na Mustafa Dotto  baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Desemba 31 siku ya jumanne katika ukumbi wa Msasani klabu  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE AKIP[IMWA AFYA
 IDDY MNYEKE AKIPIMWA AFYA YAKE

VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI 'BOXING' SASA VINAPATIKANA


VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

TASWA FC KUPAMBA BONANZA LA TWANGA PEPETA LA MWAKA MPYA VIWANJA VYA LEADERS CLUB





Na Leca Kimaro, Dar
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC kesho itapambana na timu inayoundwa na wanamuziki wa bendi ya African Stars (Twanga FC) katika mechi malaum ya kukaribisha mwaka mpya.
Mechi hiyo imepangwa kwenye viwanja vya Leaders Club inatarajia kuwa na msisimko wa aina yake ambapo baada ya mechi hiyo, bendi ya African Stars itatumbuiza jukwaani kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa mechi hiyo itaanza saa 7.00 mchana ili kutoa nafasi kwa wanamuziki wa Twanga pepeta kupanda jukwaani kutumbuiza nyimbo zao mbali mbali ikiwa pamoja na mpya mbali mbali zitakazosikika kwa mara ya kwanza.
Alisema kuwa wameamua kucheza na Twanga Pepeta kutokana na ushindani uliopo ambapo katika mechi ya mwisho, Taswa FC ilishinda kwa mabao 3-1. Alisema kuwa ushindani wa timu hizo mbili ndiyo umepelekea kufanyika kwa mechi hiyo ambapo awali, timu ya kombaini ya Jogging itapambana na timu ya makempu ya Twanga pepeta.
Meneja wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani alisema kuwa kiburudani wamejiandaa vizuri na wanamuziki wake wamepania vilivyo kuanza mwaka vyema ili kutoa burudani ya aina yake. “Hii ni sehemu ya zawadi ya mwaka mpya na wanamuziki wamepania kupiga nyimbo zote zilizotamba mwaka 2013 na pia watakaribisha maombi maalum ya nyimbo kutoka kwa mashabiki.
“Tuna albamu nyingi na nyimbo kibao zilizotamba, hivyo ni wakati wa mashabiki kufanya kile wanachokitaka kutoka katika bendi yetu, wamepewa fursa hiyo nasi tupo kambili kutimiza maombi yao,” alisema.

SHEREHE ZA RAIS KIKWETE KUKABIDHIWA RASIMU YA KATIBA





 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Warioba, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya mwisho ya Katiba mpya, Dar es Salaam leo baada ya kumaliza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi. Picha ya chini:Warioba akimkabidhi Rasimu ya Katiba, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

 Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Rasimu ya Katiba Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kulia), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya (kushoto) baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete (kulia), akimkabidhi Rasimu ya Katiba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 Baadhi ya viongozi wa vyama wakiwa katika hafla hiyo.
 Viongozi wastaafu na waasisi wa Tanzania, wakiwa wameshikilia rasimu hiyo, baada ya kukabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jana. Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Job Lusinde, Sir George Kahama, Hassan Nassor Moyo na Jaji mstaafu, Mark Bomani na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya
Baadhi ya wananchi na wanazuoni wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa Rais Jakaya Kikwete na Dk. Ali Mohamed Shein, rasimu ya mwisho ya katiba.