Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, August 2, 2009

KIFO CHA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
28/07/2009

KIFO CHA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) linasikitika kuuujulisha umma kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Ndugu Teofrid Sikazwe amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda kifupi.

Taarifa ambazo TFF imezipokea kutoka Chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Rukwa RUREFA ni kwamba Ndugu Sikazwe amekutwa na mauti hayo leo jioni majira ya saa kum.

Shemeji wa Marehemu, Philbert Umala ameieleza TFF kuwa ndugu Sikazwe alikimbizwa Katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, mjini Sumbawanga jana (Jumatatu) baada ya kulalamika kubanwa na kifua.

Ndugu Sikazwe ambaye alikuwa pia Katibu wa RUREFA kwa kipindi kirefu, juma lililopita alikuwa jijini Dar es Salaam kuhudhuria Semina iliyoendeshwa na wakufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la mpira wa miguu (FIFA) na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika Julai 20, 2009.

Ndugu Sikazwe alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kwa mara ya kwanza Desemba 27, 2004 na akachaguliwa tena wakati wa uchaguzi Mkuu wa TFF Desemba 14, 2008.

Ndugu Sikazwe alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF tangu mwaka 2004 kutokana na kuwa na taaluma ya ukocha wa mpira wa miguu na ameongoza misafara kadhaa ya timu za klabu na timu za Taifa katika michezo ya nje ya nchi.

Aliwahi kuwa kocha wa Timu ya Soka ya Ujenzi ya Rukwa na pia mara kadhaa amekuwa kocha wa timu ya Mkoa wa Rukwa katika michuano ya Kombe la Taifa.

TFF itashiriki kikamilifu katika msiba huu wa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji. Taarifa zaidi juu ya ushiriki huo zitatolewa baadaye. TFF inatoa pole kwa wanasoka Mkoani Rukwa na Tanzania kwa ujumla

Mungu aiweke roho ya marehemu Teofrid Sikazwe mahali pema peponi, Amina

Fredrick Mwakalaebela
KATIBU MKUU

No comments :

Post a Comment